1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer asema mfumo wa afya UK unahitaji 'mageuzi au ufe'

13 Septemba 2024

Onyo la waziri mkuu wa Uingereza linakuja kufuatia uchunguzi huru unaoonyesha Taasisi ya Huduma ya Kitaifa ya Afya imo "katika matatizo makubwa."

Kiongozi wa Labour Keir Starmer Akitembelea Hospitali ya Bassetlaw Kujadili Mipango ya NHS.
Starmer ameapa kutoongeza kodi kufuatia ripoti ya kutisha kuhusu hali ya Taasisi ya Huduma ya Kitaifa ya Afya, NHS.Picha: Stefan Rousseau/empics/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ameonya jana Alhamisi kuwa taasisi ya huduma ya afya ya taifa, NHS, inayofadhiliwa na serikali laazima ifanyiwe mageuzi au ife, baada ya ripoti huru kusema kuwa taasisi hiyo inayoheshimiwa iko katika "hali mbaya."

Ripoti iliyowasilishwa na Lord Darzi, mtaalamu wa upasuaji na mwakilishi wa baraza la juu la bunge la Uingereza, iligundua kuwa NHS inakabiliwa na matatizo makubwa, mwenyewe akieleza kushtushwa na alichokigundua.

Kiongozi wa Labour Keir Starmer Atembelea Hospitali ya Bassetlaw Kujadili Mipango ya NHSPicha: Stefan Rousseau/empics/picture alliance

Akijibu ripoti hiyo, waziri mkuu Starmer aliahidi kuja na mpango wa miaka 10 wa marekebisho ya taasisi hiyo, ambayo katika miaka ya hivi karibuni imetoka kuwa chanzo cha fahari ya taifa hadi ishara ya serikali na jamii zinazokabiliwa na hali ngumu.

Soma pia:  Chama cha Labour chaahidi neema Uingereza

Chama cha Starmer cha Labour kilipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mwezi Julai, na waziri mkuu huyo amesema NHS inahitaji marekebisho makubwa ili kumudu gharama zinazoongezeka za kuhudumia jamii inayozeeka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW