Keir Starmer kusaini mkataba wa ushirikiano na Ukraine
16 Januari 2025Starmer atasaini mkataba wa miaka 100 wa msaada kwa Ukraine kabla ya Rais Donald Trump kurejea madarakani Marekani.
Ni ziara ya kwanza rasmi ya Starmer tangu alipochukua madaraka Julai 2024, na inajiri wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akifanya msururu wa vikao na washirika wa nchi yake kabla ya Trump kurejea Ikulu ya White House wiki ijayo.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema mkataba huo wa kihistoria ni wa kuimarisha uhusiano wa usalama kati ya Uingereza na Ukraine.
Starmer amesema lengo la Rais wa Urusi Vladmir Putin la kuiondoa Ukraine kwa washirika wake wa karibu ni mkakati ulioshindwa.
Makubaliano hayo yanazitaka pande hizo mbili kushirikiana katika ulinzi na teknolojia ya vitani, kama vile droni za kivita, huku zikitekeleza mfumo wa kusaidia kutafuta nafaka kutoka sehemu zinazokaliwa kwa mabavu za Ukraine ambazo zinauzwa nje na Urusi.