Keita aunda serikali mpya kukabili mkwamo wa kisiasa Mali
28 Julai 2020Matangazo
Keita ambaye tangu mwezi Aprili amekuwa hana baraza la mawaziri, ameliunda baraza hilo chini ya shinikizo la Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambayo imehusika katika juhudi za kutanzua mzozo wa nchi yake.
Mawaziri watatu wamerejea katika nyadhifa zao za awali, ambao ni Waziri wa Ulinzi Ibrahima Dahirou Dembele, Waziri wa Utawala wa Kimajimbo Boubacar Alpha Bah na Waziri wa Mambo ya Kigeni Tiebile Drame.
Wapya walioingia ni Kassoum Tapo aliyeteuliwa kuwa waziri wa sheria, Abdoulaye Daffe aliyewekwa katika wizara ya fedha, na Bemba Moussa Keita ambaye amekabidhiwa wizara ya usalama wa ndani.
ECOWAS vile vile inalitaka bunge la Mali kujiuzulu na kuruhusu kuitishwa uchaguzi mpya.