1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenenisa Bekele avunja rekodi ya wanariadha wakongwe

4 Desemba 2023

Jumapili huko Valencia Uhispania kulishuhudiwa marathon ambayo Waethiopia ndio waliotawala.

Mashindano ya Dunia ya Riadha 5000m
Mwanariadha wa Ethiopia Kenenisa BekelePicha: AP

Sisay Lema raia wa Ethiopia ndiye aliyeebuka mshindi upande wa wanaume alipoandikisha muda wa saa mbili dakika moja na sekunde 48.

Lakini aliyewashangaza wengi ni mwanariadha mkongwe kutoka huko Ethiopia Kenenisa Bekele ambaye ana umri wa miaka 41 na alivunja rekodi ya mwanariadha aliye na umri wa zaidi ya miaka 40 kukimbia chini ya saa mbili na dakika tano, kwani aliandikisha muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 19.

Upande wa wanawake, Muethiopia mwengine Worknesh Degefa aliebuka kidedea kwa muda wa saa mbili dakika kumi na tano na sekunde 51.

Vyanzo: Reuters/AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW