Zambia yamzika Kaunda licha ya changamoto mahakamani
7 Julai 2021Shughuli za mazishi ya rais wa kwanza wa Zambia Kenneth Kaunda, zimenza Jumatano licha ya shauri la mahakamani lililowasilishwa na mmoja wa watoto wake wa kiume kupinga eneo anakozikwa.
Kaunda aliitawala Zambia kuanzia 1964 ilipojipatia uhuru wake kutoka Uingereza hadi aliposhindwa katika uchaguzi mwaka 1991. Alifariki Juni 17 katika hospitali ya kijeshi mjini Lusaka.
Mtoto wa Kaunda Kaweche Jumanne alipinga mahakamani mpango wa serikali kumzika baba yake katika eneo la makaburi ya marais, akisema hilo lilikuwa kinyume na matakwa yake.
Alisema serikali ilitaka kumzika baba yake katika eneo la Embassy Park dhidi ya matakwa yake, na kisha imfukuwe na kumzika katika eneo alilolitaka. Kweche Kaunda alisema wosia wa baba yake ulikuwa kuzikwa kwenye makazi yake karibu na mke wake Betty, aliefariki zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Chanzo: rtre