Uchumi
Vita ya Iran yaiongezea Kenya Airways abiria
23 Machi 2026
Matangazo
Shirika la ndege la Kenya, limesema mahitaji ya abiria ya kusafiri na ndege hiyo yameongezeka kufuatia athari zilizosababishwa na vita mashariki ya kati.
Ongezeko hilo la abiria limeripotiwa zaidi katika kanda ya Ulaya Marekani na Asia.
Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimevuruga shughuli katika sekta ya usafiri wa anga na kusababisha baadhi ya mashirika ya ndege kuongeza bei pamoja na kubadilisha ratiba zao kupunguza vituo vya kusimama katika viwanja vya ndege vya eneo la Mashariki ya kati au wakati mwingine kufuta kabisa safari zao.
Mivutano inazidi kushuhudiwa katika Jumuiya ya EAC
Shirika la Kenya Airways limesema ongezeko la wateja wake limefikia asilimia 100 kutoka asilimia 70 mwezi Januari.