Kenya: Chama Cha CORD kuwasilisha malalamiko Mahakamani
14 Machi 2013Matangazo
Kulingana na mmoja wa mawakili wa Muungano huo Eliud Owalo Cord imo mbioni kutafuta haki ya wa kenya ili wapate kuongozwa na Rais waliomchagua. Cord inadai uchaguzi mzima ulioandaliwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya ulikuwa na hitilafu nyingi.
Muda mfupi uliopita Amina Abubakar alizungumza na wakili Eliud Owalo na kwanza anaelezea wamefikia wapi kwa sasa katika hatua yao ya kuwasilisha kesi hiyo. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman