1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Kenya ilifahamu kuhusu kukamatwa Besigye: Serikali ya Uganda

23 Novemba 2024

Serikali ya Uganda imesema kuwa tukio la kukamatwa Kenya kiongozi wa upinzani Kizza Besigye lilifanywa kwa ufahamu wa serikali ya Kenya. Kauli za Uganda zimejiri baada ya Kenya kusema Nairobi imeanzisha uchunguzi.

Kiongozi wa upinzani Uganda Kizza Besigye
Besigye alikamatwa Nairobi na akasafirishwa Uganda ambako alifikishwa katika mahakama ya KampalaPicha: BADRU KATUMBA/AFP

Kauli za Uganda zimejiri siku mbili baada ya afisa mwandamizi wa Kenya kusema Nairobi imeanzisha uchunguzi kuhusu suala hilo. Msemaji wa serikali ya Uganda Chris Byaromunsi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa maafisa wa Uganda na Kenya walifahamu kuhusu kukamatwa na kuhamishwa kwa Dr. Besigye kwenda Uganda.

Soma pia: Mwanasiasa Kizza Besigye wa Uganda apandishwa kizimbani mahakama ya kijeshi

Amesema Kenya ni nchi huru na iliyo na mfumo wa kiserikali unaofanya kazi na haiwezekani mtu kukamatwa hasa mjini Nairobi na mshukiwa kusafirishwa nje ya mipaka bila ufahamu wa taasisi za Kenya.

Soma pia: Turk ataka uchunguzi dhidi ya utekaji nyara wa Besiegye

Katibu wa kudumu katika wizara ya mambo ya nje ya Kenya Korir Sing'Oei alikitaja kisa hicho kuwa cha kusikitisha. Alisema hakikuwa kitendo cha serikali ya Kenya wala cha maafisa wa usalama wa nchi hiyo. Uganda imekabiliwa na shutuma za kimataifa kufuatia kutekwa kutoka Nairobi kwa Besigye, aliyefikishwa katika mahakama ya Kampala Jumatano.