1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yakabiliwa na duru mpya ya maandamano

19 Julai 2023

Kenya inakabiliwa leo na duru mpya ya maandamano licha ya serikali kuonya kwamba haitavumilia machafuko zaidi baada ya maandamano ya awali kusababisha vifo vya watu zaidi ya 10.

Waandamanaji nchini Kenya wakifanya maandamano jijini Nairobi mnamo July 12 2023
Maandamano ya ghasia nchini KenyaPicha: Luis Tato/AFP

Maeneo kadhaa ya nchi yakiwemo mitaa mbalimbali ya Nairobi na Kisumu kwa sasa yanashudia makabiliano kati ya waandamanaji na polisi. Polisi wanawafyatulia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji wanaoonekana kuwasha moto matairi barabarani.

Upinzani umeapa kufanya maandamano kwa siku tatu mfululizo

Upinzani umeapa kufanya maandamano kwa siku tatu mfululizo dhidi ya serikali ya Rais William Ruto, na kusababisha jumuiya ya kimataifa kujiunga katika kutoa wito wa kupatikana suluhisho la kisiasa katika mzozo huo. Shule za kutwa na maduka yamefungwa katika mji mkuu wa Nairobi na miji mingine, huku waandamanaji wakihimizwa kubeba sufuria na kuingia mitaani.

Hii ni mara ya tatu Raila Odinga aandaa maandamano makubwa

Hii ni mara ya tatu ndani ya mwezi huu kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuandaa maandamano makubwa dhidi ya serikali anayosema si halali na inahusika na mgogoro wa kupanda gharama ya maisha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW