1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Juniour Starlets mbioni kusaka Kombe la Dunia

11 Oktoba 2024

Wakati mataifa mengine ya Afrika yamefanikiwa kwa muda mrefu katika ngazi ya kimataifa kwenye soka la wanawake, Kenya imekuwa nyuma. Lakini kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 kunatoa matumaini.

Kenya Nairobi | Mazoezi | Timu ya kandanda ya wachezaji  U17- wasichana
Harambee Junior Starlets wakiwa mazoezini kujiandaa kwa mashindano ya Kombe la Dunia wachezaji chini ya miaka 17 yatakoandaliwa Jamuhuri ya Dominika.Picha: CHRIS OMOLLO/Shengolpixs/Imago Images

Msisimko na hisia zilidhihirika baada ya Kenya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake wa chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza. Ilikuwa zaidi ya hatua muhimu katika michezo, ilikuwa ni mwanga wa matumaini kwa wasichana wadogo kote nchini.

Kocha mkuu wa kikosi hicho Mildred Cheche ameiambia DW kwamba wengi wao, wanatoka kwenye asili zenye hadithi za kusikitisha, na soka kwao ni kila kitu. Hawachezi tu kwa ajili ya kujifurahisha lakini ili kupata riziki.

Cheche amesema "Kwa Kenya, tumeanza kuwa na msimamo muda mfupi tu nyuma. Itachukua muda, lakini nadhani tuko kwenye njia sahihi kufikia kiwango sawa."

Ushindi wa jumla wa mabao 5-0 dhidi ya Burundi uliiwezesha Kenya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia la mwaka huu huko Jamhuri ya Dominika itakayoanza Oktoba hadi Novemba.

Mafanikio ya Junior Starlets yalibadilisha mitazamo ya kile kinachoweza kufikiwa na kuwafanya wengi kutambua kuwa taaluma ya michezo, iwe kama wachezaji, makocha, waamuzi au wasimamizi wa michezo yanawezekana.

Soma pia: Kenya imeivunja bodi ya soka kwa tuhuma za rushwa

Kenya ilitatizika kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa ufadhili, usimamizi duni, na ukosefu wa vifaa vya kutosha vya mafunzo kwa timu za wanawake. Ukosefu wa uwekezaji ambao kocha Cheche alikuwa ameuzoea kama mchezaji ulidhihirika zaidi alipoingia kwenye ukocha mwaka wa 2011.

Kandanda inakabiliwa na vikwazo vikubwa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa muundombinu mzuri, hakuna ufikiaji wa vifaa, kimsingi hakuna vifaa.

 

Kenya ilibaki nyuma ya mataifa mengine ya Afrika

Kocha wa Harambee Junior Starlets Mildred Cheche akiikiandaa kikosi cahke kwa Kombe la Dunia U17.Picha: CHRIS OMOLLO/Shengolpixs/Imago Images

Wakati soka la wanawake nchini Kenya lilitatizika kuchukuliwa kwa uzito, Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) liliunda miundombinu ya kandanda ya wanawake tangu miaka ya 1990, ili kutambua vipaji mapema na kuvikuza.

Ushiriki wa mara kwa mara wa Super Falcon katika mashindano ya kimataifa ya FIFA uliwapa wachezaji uzoefu muhimu dhidi ya viwango tofauti vya wapinzani. Wachezaji kama Asisat Oshoala wakawa majina ya nyumbani, na kuwatia moyo wasichana wachanga kufuatilia soka.

Wakati huo huo, nchini Kenya ukosefu wa wachezaji wa kuigwa wa kandanda wa kike inaonekana imekuwa kikwazo. Lakini sasa mabadiliko yanatokea.

 

Ulaya ndio lengo la kizazi kipya

Lengo la wachezaji wakike ni kujiunga na klabu nje ya nchi hasa Ulaya. Pichani Asisat Oshoala alipoichezea klabu ya uhispania, Barcelona, 2023.Picha: David Ramos/Getty Images

Kwa mfano nahodha Elizebeth Ochaka wa Juniour Starlets amekuwa na kaya inayomuunga mkono, imekuwa muhimu katika ukuaji wake kama mchezaji na uzoefu wa hivi karibuni wa tamaduni na vyakula tofauti umemfungua macho beki huyo kwa uwezekano wa kutambulika kimataifa.

"Ningependa kujiunga na klabu nje ya nchi kwa sababu nimeona Ulaya kuna timu ambazo ni nzuri, Ningependa kujiunga na mmoja." Ochaka alisema.

"Wachezaji wetu wametoka kucheza katika michezo ya shule, hadi mashindano ya kikanda na sasa wako kwenye hatua ya Kombe la Dunia. Kwao nafasi ya sasa ya kufuatiliwa na timu kubwa ni fursa ya kubadilisha maisha." Alisema kocha Cheche.

Kocha mkuu Cheche pia anaamini kuwa, kwa timu hiyo, kufika hatua ya Kombe la Dunia kutawawezesha wachezaji kuonyesha vipaji vyao kwa watazamaji wengi zaidi.

Kenya inakabiliwa na wapinzani watatu wakali katika awamu ya makundi, ikichuana na washindi mara mbili Korea Kaskazini, washindi wa pili wa 2018 Mexico na Uingereza.

Ingawa mafanikio ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la wachezaji chini ya miaka 17 yalikuwa makubwa kwa Kenya, Cheche hakatai kuwa timu yake inaweza kufanya maajabu katika mashindano hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW