Kenya kitovu cha mafuta Afrika Mashariki?
17 Januari 2014Usafirshaji wa mafuta pia huenda ukaanza mwaka 2019, ambapo kampuni hiyo inakadiria kuwa huenda yakapatikana jumla ya mapipa milioni 600 katika eneo hilo.
Kampuni hiyo ya uchimbaji mafauta imesema kufuatia ugunduzi huo wa mafauta, mradi wa usafirishaji unategemea kugharimu jumla za dola bilioni 4 za Marekani, lakini kwanza hatua muhimu kama vile kuboresha miundo mbinu na kuwajengea uwezo wananchi zinapaswa kuanza sasa.
Kuna uwezekano wa kupatikana mafuta zaidi, anasema Wood Mackenzie, mashauri wa mradi huo na kuongeza kuwa ugunduzi wa mafauta katika mabonde mawili ya Lokichar nchini Kenya na jingine la Uganda yatafanya upatikanaji wa jumla ya mapipa bilioni 4 za mafuta, ambapo hadi sasa mapipa bilioni 1.6 yamekwishapatika Uganda.
Amesema mataifa hayo mawili yana uwezo wa kuzalisha mapipa 500,000 kwa siku, na hivyo kusaidia kukuza uchumi katika ukanda wa Jangwa la sahara kwa asilimia 8 kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 6.2 cha ukuaji wa uchumi.
Wananchi kunufaika?
Hata hiyo wasi wasi ni juu za kampuni hiyo kuwa makini katika mpango wa ke wa kuanza kuchimba mafuta Kenya, kutokana na kampuni hiyo kwa kushirkiana na kampuni za uchimbaji mafuta Afrika kusitisha kufanya kazi kwa wiki mbili mwaka jana baada ya wananchi wa maeneo hayo kufanya maandamano kudai faida watakazopata kutokana na mradi huo.
Nchini Uganda kampuni hiyo ya Tullow imelalamikiwa kwa kuchelewa kufanya uzalishaji wa mafuta, ambayo yaligunduliwa tangu mwaka 2006, lakini ilijitetea kuchelewa kutokana na matatizo ya kisiasa.
Hata hivyo kwa Catriona O'Rourke mchambuzi mwandamizi wa masuala ya Jangwa la Sahara anasema Kenya imepokea kwa furaha juu ya taarifa za kusafirisha mafuta kutoka eneo lake na itafaidika zaidi ikilinganishwa na Uganda, kwa kuwa itatakiwa kujenga tu bomba la usafirishaji katika eneo la Bahari.
Kampuni hiyo imsema ni matarajio yake kuanza usafirisha mafuta kuanzia mwaka 2019,ikiwa hakutakuwa na vikwazo vya kisiasa, ambapo uchimbaji rasmi umepangwa kuanza mwaka 2006.
Pia kuna hofu ya kuwepo kwa vikwazo zaidi ya vile vya kisiasa vinavyoweza kuchelewesha mradi huo, ingawa Kenya kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki inapaswa kujifunza juu ya uvumbuzi wa biashara mpya kutokana na uwezo wake mdogo katika kuendesha mradi huo mkubwa kama huo wa uchimbaji mafuta.
Mradi kugharimu dola bilioni 4
Mradi huo mkubwa wa kusafirishaji mafuta utakaogharimu Dola bilioni 4 za Marekani kwa kuunganisha kutoka Uganda na Kenya ni sawa na mara tano ya makadirio ya bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka 2013/2014.
Afisa mmoja wa Kenya amesema ujenzi wa mradi huo utachukua muda mrefu, hivyo wananchi wanapaswa kuwa na subira, huku baadhi ya wanasiasa wakionekana kuchoshwa na taratibu za serikali kupitia muswada mpya kusimamia sekta ya mafuta wenye lengo la kuvutia zaidi wawekezaji.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayosimamia sekta ya nishati, Jamleck Kamau amesema wizara husika inayosimamia masuala ya marekebisho ya sheria inafanyia kazi muswada huo na kukiri kuwa, zoezi hilo linakwenda taratibu.
Mwandishi: Flora Nzema/RTRE
Mhariri: Saumu Yusuph Mwasimba