1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kizani baada ya tangazo la kifo cha Raila Odinga

Musa Navie 15 Oktoba 2025

Kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Amolo Odinga kimeibua majonzi nchini Kenya, wafuasi wa kiongozi huyu wanaeleza hisia zao kutokana na kuondokewa na kinara huyo wa upinzani.

Kenya Nairobi | Raila Odinga
Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga afariki dunia nchini India akiwa na umri wa miaka 80Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Mapema asubuhi siku ya jumatano, minongono kuhusu kifo cha Raila Amolo Odinga ilisambaa mitandaoni wengi wasijue uhakikika wa yaliyokuwa madai ya kufariki kwa kiongozi huyo wa upinzani.

Jijini Kisumu, minongoni hii ilitawala sehemu za mitaani, biashara, makundi ya watu yakionekana katika sehemu za mabunge ya wananchi, miongoni mwa maeneo mengine ya jumla, nduru zikisikika, baadae majira ya saa nne asubuhi ilikuwa dhahiri kuwa, habari kuhusu kifo cha Odinga zilikuwa za kweli na hapo wakaazi jijini Kisumu walikafurika barabara za mitaa ikiwemo Kondele na katikati ya mji kuomboleza kifo cha kinara huyu.

Kwa mabango na nduru, walimemiminika, wahudumu wa bodaboda wamebeba matawi, akina mama kwa wanaume wakitawaliwa na nduru, majonzi na kauli mbali mbali na kuelekea hadi ikulu ndogo ya Kisumu kwenye maombolezi yao.  

Raila atakumbukwa kwa kuondoa uongozi wa chama kimoja Kenya

Raila Amollo Odinga ambaye nyumbani kwao ni jimbo la Siaya na mwenye makao yake katika vilima vya Riat jimbo la Kisumu alizaliwa katika hospitali ya kanisa la kimishenari la Maseno mnamo tarehe 07 Januari mwaka 1945, babake Jaramogi Oginga Odinga makamu wa rais wa kwanza wa Kenya na mamake Mary Juma Odinga.

Katika elimu yake, Raila Odinga alisomea katika shule ya msingi ya Kisumu na baadae shule ya msingi ya Maranda kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Maranda na kusomea katika taasisi ya Herder ya Ujerumani, mwaka 1965 alijiunga na chuo cha kiufundi cha Magderburg Ujerumani akifuzu na shahada ya masters katika Uhandisi wa mitambo na kurejea nchini Kenya mwaka 2070.

Atakumbukwa pakubwa kwa kuwa miongoni mwa wanasiasa walioshinikiza kuondolewa kwa uongozi wa chama kimoja nchini Kenya na kuuondoa uongozi wa chama cha KANU katika kampeni alizoziongoza mnamo mwaka 2002 zilizompa ushindi rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki.

Raila aliaga dunia akipokea matibabu India

#Mwaka 2007 ghasia za uchaguzi mkuu ziligubika taifa mazungumzo yaliyoongozwa na Kofi Anan zikipelekea maridhiano yaliyounda serikali ya nusu mkate Raila akichukua wadhifa wa waziri mkuu. Kabla ya wadhifa wa Uwaziri Raila amehudumu kama mbunge wa eneo bunge la Lang'ata Nairobi na wadhifa wa Uwaziri.

Mwaka 2010 alipigia debe uundwaji wa katiba mpya ya Kenya na kuungana na rais mstaafu Uhuru Kenyatta maarufu handshaki ushirikiano uliodumu hai kura ya uchaguzi mkuu mwaka 2022 ambapo alishindwa na rais wa sasa William Ruto ambaye baadae alimhusisha kwenye serikali ya Ushirikiano maarufu Broadbased 2024.

Raila amefariki akipokea matibabu nchini India akiwa na umri wa miaka 80.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW