1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Kufurika kwa wafanyibiashara kutoka China

Shisia Wasilwa
28 Februari 2023

Wafanyabiashara jijini Nairobi nchini Kenya wameandamana mchana kutwa jijini humo kwa kile wanachokitaja kuwa ni kufurika kwa wafanyibiashara kutoka China nchini humo. Sasa wanaitaka serikali iyalinde maslahi yao.

Kenia | Präsident William Ruto
Picha: James Wakibia/ZUMAPRESS/picture alliance

Makumi kwa mamia ya wafanyibiashara hao waliandamana kutoka katikati ya jiji kwa amani hadi kwenye afisi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua, wakiomba serikali kuingilia kati suala hilo. Waandamanaji hao waliokuwa na mabango, huku wakipuliza tarumbeta, kwa wakati mmoja walikutana na maafisa wa polisi ambao walikuwa wakilinda amani...Mara nyingi maandamano yanapofanyika, wezi na wahalifu huchukua fursa hiyo na kutekeleza maovu. Walizuia barabara ya Harambee Avenue iliyoko mbele ya ofisi ya Naibu Rais huku polisi wakiwalinda.

Wataalamu waonya kuhusu athari za maandamano

Waandamanaji jijini NairobiPicha: AP

Hata hivyo baadhi ya wataalamu wanaonya kuwa maandamano haya yanaweza kuwa na athari hasi kwa dhana ya uhuru wa kufanya biashara ulimwenguni.

Maandamano hayo yanajiri siku moja kabla ya mkutano wa wafanyabiashara hao na Naibu Rais Rigathi Gachagua. Mkutano huo ukilenga kujadili suala la ongezeko la wageni kufanya biashara nchini Kenya hasa raia wa kutoka Pakistan na Wachina. Wafanyibiashara wanahisi kuwa soko lao limetekwa nyara na wageni. Wafanyabiashara hao waliwasilisha malalamiko yao kwa Naibu Rais Gachagua kwa mara ya kwanza juma lililopita wakitisha kufanya maandamano na Gachagua aliapa kuwalinda. Maandamano hayo pia yanajiri siku chache baada ya kufungwa kwa duka kubwa la jumla jijini Nairobi lililokuwa linamilikiwa na raia wa China.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW