1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kupambana na magenge ya uhalifu

Wakio Mbogo9 Machi 2022

vikosi vya usalama Kenya vimetakiwa kutowapa nafasi wahalifu ambao kwa kiwango kikubwa hutishia usalama wa raia na mali zao katika maeneo ya Baringo na Pokot Magharibi ambapo Operesheni hiyo inafanyika.

Uhuru Kenyatta Präsident Kenia Rede Parlament Nairobi
Picha: Simon Maina/AFP via Getty Images

Wizara ya usalama wa ndani imetangaza Operesheni kali eneo la mipakani mwa Baringo na Pokot Magharibi ambapo watu wengi wameuawa na mali nyingi kuharibiwa kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya kihalifu.

 Akizungumza huko Muchongoi Baringo, Kamishna mkuu wa eneo la bonde la ufa Maalim Mohammed ametangaza kwamba polisi 80 maalum wa akiba wamepelekwa maeneo hayo pamoja na zana za kivita." kwakushirikiana na waziri tunataka kuhakikisha kuwa maafisa wetu wamepelekwa, tunahitaji kujua wangapi wameshikwa" Alisema Kamishna mkuu Mohammed

Soma pia:Kenya yatangaza operesheni mpya ya usalama

Ujumbe huu wa maafisa wa usalama ulifika Baringo baada ya kutwa nzima ya makabiliano ya risasi kati ya polisi na wahalifu. Hisia za wasiwasi na majonzi zimetanda kwenye eneo hilo, huku mamia ya wakaazi wakionekana wakiyahama makaazi yao kwa kuhofia maisha yao.

Wanafunzi wahamishwa ili kukamilisha mitihani yao

Ni hali iliyotatiza zoezi la kuwahamisha watahiniwa walioanza mitihani yao ya kitaifa siku ya jumatatu hadi maeneo salama, kwani watahiniwa wenyewe waliandamana na jamaa zao kujiokoa.

Hata hivyo Kamishna mkuu Mohammed anathibitisha kuwa waliwatafuta na kuhakikisha watahiniwa wote wamefika ili kufanya mitihani. Amesema wamehakikisha wameshirikiana na wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa salama ili kukamilisha mitihani yao shuleni "watoto wametafutwa vilivyo." alisisitiza Kamishna Mohammed

mwalimu akisismamia watahiniwa NairobiPicha: Donwilson Odhiambo/ZUMA/picture alliance

Soma pia:Wafungwa waadhimisha siku ya wanawake Kenya

Kinachotia wasiwasi ni mazingira magumu wanayojipata wanafunzi hao, na kwamba inawabidi wafanyemitihaniyao chini ya hali isio kuwa ya kawaida kama wanafunzi wengine katika maeneo ya nchini hiyo.

Viongozi wa maeneo hayo wameitaka serikali kutoa suluhisho la haraka ili kuhakikisha hali ya usalama inarejea kwa wakaazi katika eneo hilo la Baringo na Pokot Magharibi.Walisema sasa umefika msimu wa kulima na wakaazi wanahitaji kuendeleza shughuli zao za kilimo kwa amani na utulivu "naomba serikali iwasaidie kulima mashamba hawa watu fedha ipo." Alisema Mbunge wa Baringo Kusini Charles Kamuren.

Serikali yaonya wanaomiliki silaha kinyume cha sheria

Awali wiazara ya usalama wa ndani ilieleza kwamba ina orodha ya majina ya watu wanaomiliki silaha kunyume na sheria katika maeneo hayo, hatua ambayo imetoa wito kuzisalimisha mara moja.Operesheni hii inatarajiwa kuimarisha usalama katika maeneo hayo ili kuwawezesha wakaazi kurejelea maisha yao ya kawaida.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW