Kenya kuuza mafuta nje
2 Agosti 2019Matangazo
Hii itakuwa shehena ya kwanza ya mafuta ghafi yatakayouzwa nje ifikapo kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka 2019.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni ya Tullow, mafuta hayo tayari yameshasafirishwa hadi mjini Mombasa.
Tullow Oil, iliyo na visima vya mafuta katika Kaunti ya Turkana, imekuwa ikisafirisha mapipa 600 ya mafuta kwa siku hadi eneo la pwani ya Kenya ila tangu mwezi wa Mei imeiongeza idadi hiyo na kufikia mapipa 2,000.
Hata hivyo maelezo ya kampuni iliyoingia ubia na Kenya hayajakuwa bayana.
Kenya iligundua hifadhi ya mafuta mnamo 2012 kwenye Bonde la Lokichar na inakisiwa kiasi ya mapipa milioni 560 huenda yakapatikana baada ya eneo hilo kuchimbwa kikamilifu.
Thelma Mwazdaya/DW Nairobi