1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Mfumo wa elimu na mtihani wa 8-4-4 wafikia kikomo

30 Oktoba 2023

Nchini Kenya mfumo wa elimu na mitihani wa 8-4-4 umefikia kikomo huku wanafunzi wa shule ya msingi wakifanya mtihani wa mwisho wa kumaliza darasa la nane, KCPE.

Kiasi ya wanafunzi milioni 1.2 wanafanya mtihani wa KEPSEA mwaka huu.
Kiasi ya wanafunzi milioni 1.2 wanafanya mtihani wa KEPSEA mwaka huu.Picha: Getty Images/AFP/S. Maina

Baada ya sasa, wanafunzi wa shule ya msingi watafanya mtihani wao wakiwa darasa la sita wa KEPSEA chini ya mfumo wa 2-6-6-3.

Mfumo huu mpya unajikita zaidi katika kukuza vipaji na uwezo wa mwanafunzi badala ya kupita mitihani.Thelma Mwadzaya anaarifu zaidi kutoka Nairobi.

Baada ya kiasi ya miongo minne,mfumo wa elimu wa 8-4-4 nchini Kenya unafikia kikomo.

Kiasi ya wanafunzi milioni 1.4 wa shule ya msingi wanafanya mtihani huu wa mwisho wa KCPE utakaokamilishwa Jumatano wiki hii.

Mapema hii Jumatatu akiwatembelea watahiniwa wa shule ya msingi ya Kikuyu katika kaunti ya Kiambu, Rais William Ruto aliwahakikishia kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuimarisha hali ya elimu nchini Kenya.

Kimsingi, wanafunzi watakuwa wakifanya mtihani wao wa kwanza wa kitaifa wakifika darasa la sita.Picha: DW/Shisia Wasilwa

Mfumo mpya wa 2-6-6-3

Wizara ya Elimu itafuata mfumo mpya wa 2-6-6-3 ambao unajikita zaidi kukuza vipaji na uwezo wa mwanafunzi badala ya kupita mitihani.

Seneta wa Kaunti ya Uasin Gishu kizimbani kujibu mashtaka juu ya mipango wanafunzi kusoma Finland

Kimsingi, wanafunzi watakuwa wakifanya mtihani wao wa kwanza wa kitaifa wakifika darasa la sita.

Wakati huohuo, usalama uliimarishwa kote nchini hasa kwenye maeneo ambayo yanatatizwa na wapiganaji na uvamizi kama vile kaskazini.

Mtihani mpya wa KEPSEA wa shule za msingi utatumika kutathmini na kufuatilia utendaji wa mwanafunzi na wala sio kuamua iwapo ataendelea na masomo hadi darasa la saba ambalo ndio mwanzo wa awamu ya vidato vya chini vya sekondari.

Ifahamike kuwa kikundi cha kwanza cha wanafunzi wa KEPSEA kilitahiniwa mwaka uliopita wa 2022.

Wanafunzi watatahiniwa masomo matano pekee

Kiasi ya wanafunzi milioni 1.2 wanafanya mtihani wa KEPSEA mwaka huu.

Wadau wote katika jamii wameshauriwa kushirikiana na taasisi za usalama na elimu ili kuhakikisha zoezi la mtihani linapita salama. Wilberforce Kilonzo, naibu kamishna wa kaunti ya Kisii na ameeleza kuwa jamii imefahamishwa.

Kwenye mfumo mpya, wanafunzi watatahiniwa masomo matano pekee ijapokuwa watasoma 12.Picha: DW/Shisia Wasilwa

Wanafunzi hawatatahiniwa kwenye masomo ya Hesabu, Kiingereza, Kiswahili, Sayansi, Elimu ya jamii na dini kwenye mtihani wao wa kwanza wa kitaifa.

Wanafunzi kadhaa Kenya huenda wasifanye mitihani ya taifa

Kwenye mfumo mpya, wanafunzi watatahiniwa masomo matano pekee ijapokuwa watasoma 12.

Mtihani huo mpya utachukua 40% ya matokeo yote ya mwanafunzi na 60% iliyosalia itatokea kwenye utendaji wake darasani.

Mitihani ya KCPE NA KEPSEA inakamilika Jumatano, Novemba mosi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW