1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mikasa ya moto mashuleni yazusha hofu kwa wanafunzi

11 Septemba 2024

Wadau katika sekta ya elimu Kenya wamehusisha uoga wa mitihani ya kitaifa, msongo wa mawazo na ukosefu wa ushauri nasaha kutoka kwa waalimu na wazazi vinazochangia misururu ya mikasa ya moto katika shule.

Shule ya msingi ya Hillside iliyoko Nyeri
Shule ya msingi ya Hillside iliyoko NyeriPicha: AP Photo/picture alliance

Baada ya mkasa wa moto katika shule ya bweni ya Hillside Endarasha jimbo la Nyeri eneo la Kati nchini Kenya uliosababishwa vifo vya wanafunzi 21, shule kadhaa zimeripoti mikasa ya moto ikiwemo shule ya sekondari ya wasichana ya Isiolo ambapo bweni la wanafunzi wa kidato cha kwanza liliteketea kwa moto. Kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu, wanafunzi 3 wamejeruhiwa. Mbali na shule hii, shule zingine tano ikiwemo ya wavulana yaIsiolo iliyopo mita chache na wenzao wa kike zimeteketea kwenye majimbo ya Bungoma, Meru, Pokot Magharibi.

Wadau wa elimu wakiwemo walimu kutoka eneo la magharibi mwa Kenya na mashariki mwa taifa wakianda vikao majimbo ya Bungoma, Makueni na Kongamano la Elimu jimbo la Kisii, wanahusisha mgomo wa walimu wa shule za sekondari ulioshuhudiwa katika baadhi ya maeneo nchini kuchangia mikasa ya wanafunzi kuchoma shule, takribani shule sita zikiripotiwa kuchomwa moto katika muda wa chini ya wiki moja wakitaka mabadiliko kufanyiwa usimamizi wa baadhi ya shule na serikali kuunda jopo kazi la kuchunguzi kiini cha mikasa hiyo.

Shule ya msingi ya Hillside iliyoko NyeriPicha: AP Photo/picture alliance

Katika mahojiano na mwalimu wa shule ya sekondari ya Gemeni jimbo la Vihiga, magharibi mwa Kenya, Shipendi Asega Benard anasema ni muhimu walimu kujenga uhusiano mwema na wanafunzi na idara za ushauri nasaha kuimarishwa ili kuwawezesha kujieleza kikamilifu.Wazazi wasubiri hatma ya watoto shule iliyowaka moto Kenya

"Sidhani kama itakuwa na manufaa, lakini kwa kiwango kikubwa huwa wanaunda majopo haya ambayo nimeshuhudia kwa muda mrefu kwamba suluhisho huwa halipatikani kwa njia inayofaa, kwa hivyo napendekeza pawe na tofauti, pengine kila shule ishugulikie suala hili kwa karibu. Mimi kwa upande mmoja naona kama majopo kazi haya majukumu wanayotoa huwa yanasahaulika baada ya moto kupoa, wanastahili kufuatilia kwa karibu."

Mwalimu Steven Ochieng wa Shule ya Wasichana ya Rae jimbo la Kisumu anasema ikiangaliwa kwa karibu mikasa mingi ya moto shuleni huongezeka ndani ya muhula wa tatu akihusisha hali hii na hofu ya mitihani ya kitaifa ambayo huamua wanafunzi kujiunga na darasa linalofuata na mitihani ya kitaifa.Ruto atangaza siku tatu za maombolezo kufuatia vifo vya wanafunzi 17

Anapendekeza wanafunzi kupewa ushauri nasaha kuanzia kwa wazazi kuwaelewesha kuwa mikasa ya moto ina gharama za kiuchumi na maisha.Wanafunzi 17 wafariki kwa kuteketea moto Kenya

"Wanajaribu kuwashawishi wenzao ili waweza kurudi nyumbani wakiwa na matumaini kwamba mtihani unaweza kuhairishwa, pili wanafunzi wengi wameingilia matumizi ya mihadarati hivyo wanakuwa na utovu mwingi wa nidhamu na swala hili pia linachangia pakubwa uteketezaji wa shule.''

Usalama wa wanafunzi katika shule za bweni Kenya

02:37

This browser does not support the video element.

Mtaalamu wa afya ya umma na utafiti Amon Otieno wa shirika la masuala ya afya ya akili la Smart Dapper anasema utafiti waliofanywa kwa ushirikiano na chuo kikuu Nairobi, ulibaini kuwa, matukio ya mikasa ya moto katika shule nchini Kenya yanachangiwa na matatizo ya akili ikiwemo shinikizo la kuandikisha matokeo bora kwa wanafunzi, wakiishia kukabiliwa na  msongo wa mawazo na kuwa na Kiwewe ambayo yanatoa msukumo wa kusababisha kuchoma shule ikizingatiwa waliyoyashuhudia maishani.

Anapendekeza wizara ya elimu kuwaajiri wataalamu wa ushauri nasaha kando na walimu wanaowafundisha wanafunzi pia kuwa ndio wanaotoa ushauri nasaha ilivyo kwa sasa.Kenya: Wanafunzi 70 hawajulikani walipo kufuatia mkasa wa moto

"Wanafunzi wote sio sawa kwa sababu kuna wale ambao wanapitia changamoto mbalimbali, mtu anajiona yuko na hali duni akijilinganisha na mwingine, halafu kuna mzazi anakuambia nenda usome na upate alama ya A ama B na isiwe chini ya hiyo. Wanafunzi wengi ambao tumeongea nao wanasema shule ni kama jela"

Baadhi ya taratibu zilizotolewa na wizara ya elimu nchini Kenya kufuatia mapendekezo ya jopo kazi la wataalamu ni kila shule kuwa na vifaa vya kuzima moto, sehemu za kukimbilia moto unapoibuka na mbinu za kitaalamu za uokoaji kwa watakaofungiwa na moto.

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi