1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya na Somalia zakubaliana kurekebisha mahusiano

15 Novemba 2019

Kenya na Somalia zimekubaliana kurekebisha mahusiano yao na kuanza tena kutoa vibali vya kusafiri kwa raia wao baada ya msuguano wa muda mrefu kuhusu mpaka wa baharini ambao ulitia doa uhusiano wa mataifa hayo jirani.

Kenia Nairobi Besuch Somalischer Präsident
Picha: picture-alliance/AP Images/K. Senosi


Makubaliano hayo yametangazwa jana na ofisi ya rais nchini Kenya kufuatia mkutano kati ya rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed mjini Nairobi.

Viongozi hao wamesisitiza juu ya uhusiano wa dhati uliopo kati ya Kenya na Somalia na wamekubaliana kutafuta njia za kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia.

Hata hivyo taarifa hiyo haikutaja lolote kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia juu ya ukanda wa bahari ya Hindi unaodhaniwa kuwa na hifadhi ya mafuta na gesi ambao kila upande unadai umiliki.