1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKenya

Kenya na Uganda kusuluhisha mzozo wa Ethiopia na Somalia

30 Novemba 2024

Rais wa Kenya William Ruto amesema hii leo kwamba yeye na Rais wa Uganda Yoweri Museveni watasaidia kupatanisha mzozo kati ya Ethiopia na Somali, uliotishia utulivu wa kikanda.

Kenya Nairobi 2024 | Rais wa Uganda Museveni na Ruto wa Kenya
Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais wa Kenya William Ruto wanalenga kujitumbukiza kwenye suluhu ya mzozo kati ya Somalia na EthiopiaPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Ruto ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba hii ni kwa sababu usalama wa Somalia unachangia kwa kiasi kikubwa katika utulivu wa kikanda, na kuboresha mazingira ya uwekezaji na wafanyabiashara.

Uturuki imejaribu mara kadhaa kusuluhisha mzozo huo lakini haijafanikiwa.

Ethiopia yenye maelfu ya wanajeshi nchini Somalia wanaopambana na waasi wenye mafungamano na al-Qaeda imejikuta katika mzozo na serikali ya Mogadishu kufuatia mipango yake ya kujenga bandari katika jimbo lililojitenga la Somaliland, ili badala yake iweze kuisaidia kutambuliwa kimataifa.

Somalia inaipinga vikali hatua hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW