Kenya: Nafasi kwa wawekezaji wa Ujerumani
27 Septemba 2012Hali hii inawavutia wawekezaji wa kimataifa. Hata hivyo wafanyabiashara wa Ujerumani hadi sasa wamekuwa wakijizuwia kuingia katika soko hili. Lakini hali hiyo inakaribia kufika mwisho, kwa kuwa katika mji mkuu Nairobi linafanyika jukwaa la kiuchumi kati ya Ujerumani na Kenya linaloanza hii leo (26.09 hadi Novemba 28).
Wakati ukizungumzia kuhusu uwekezaji nchini Kenya ,si kwamba unaizungumzia tu Kenya pekee yake. Kwasababu nchi hiyo ni njia ya kuingia wawekezaji kutoka nje kwa eneo lote la Afrika mashariki. Nchi hiyo ina bandari katika mji wa Mombasa na bandari hii haitumiki tu na nchi ya Kenya yenyewe binafsi , bali pia kwa mataifa jirani ambayo bidhaa zake zinasafirishwa kwa meli.
Hata maendeleo yaliyopigwa na uongozi wa nchi hiyo na uwekezaji katika miundo mbinu yanawavutia wawekezaji.
Hata hivyo wafanyabiashara wa Ujerumani hadi sasa wamekuwa wakijizuwia kuwekeza nchini humo. Lakini sasa chama cha wenyeviwanda nchini Ujerumani na wafanyabiashara wameanzisha ofisi maalum mjini Nairobi. Ingo Badoreck anawakilishi maslahi ya kiuchumi ya Ujerumani nchini humo. Kwake yeye anasema uwezo wa Kenya haujawekwa katika hali halisi.
"Tumepata ukuaji mkubwa hapa nchini Kenya, hali ambayo haijatambuliwa na uchumi wa Ujerumani. Hapa tuna miradi mikubwa ya miundo mbinu na pia katika sekta ya afya, katika sekta nishati inayoweza kutumika tena, na hii ni miraji ambayo inapendelewa pia na wawezekaji wa kati".
Wafanyabiashara wakubwa wa sekta ya nishati tayari wamekuwa wakifanyakazi nchini Kenya, kama vile kampuni la kemikali la BASF, ambapo kilimo na sekta ya ujenzi vimekuwa sehemu muhimu ya ziada kwa makampuni haya nchini Kenya. Kampuni linalotengeneza vipodozi la Baiersdorf linazalisha bidhaa kwa ajili ya soko la eneo lote la Afrika mashariki. Hii imewezekana kutokana na idadi kubwa ya wafanyakazi ambao wana elimu ya kutosha katika suala hilo. Kwa ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia tano , nchi hiyo imekuwa injini muhimu ya uchumi wa Afrika mashariki.
Drago Buzuk ana matumaini makubwa zaidi kwa mwaka ujao. Yeye anawakilisha kampuni la "German Teknology Solutions", ambalo linajumuisha makampuni 30 ya Ujerumani ya kiwango cha kati. Makampuni yote hayo yana matumaini , kuwa mataifa ya Afrika mashariki kwa kuwa na utajiri wa maliasili yanaweza kukua na kuwa kama China katika muda wa miaka 20 ijayo. Lakini unatokea pia ushindani kutoka eneo hilo, anasema Buzuk.
"Tatizo ni kuwa uchumi wa Ujerumani umetelekeza eneo hilo kwa kiasi kikubwa na hapa kuna wafanyabiashara wachache kutoka Ujerumani, ambao wanaweza kushughulika na shughuli za kawaida za kila siku na kuweza kuongoza hatua za maendeleo.Kwa upande wa Wachina hilo ni tofauti. Pia kuhusu suala la upatikanaji wa fedha , wanaodhibiti ni Wachina ambao wako haraka kufanya hivyo".
Mwakilishi wa mambo ya uchumi Ingo Badoreck anapambana na ushindani huo kutoka Asia kwa kujiamini.Kwake yeye suala ni kuhamisha utaalamu.
"Hicho ndio kitu muhimu, ambacho washirika wetu wa Asia hawakiwezi. Sio tu kwamba tunauza bidhaa zetu hapa na bidhaa zetu kuziingiza katika soko la Kenya, lakini tunajaribu pia kuingiza utaalamu na ujuzi wetu kwa watu wa hapa".
Tunawezaje basi kuchochea uwezo wa wafanyabiashara wa Ujerumani kuelekea Afrika? Kazi hiyo inafanywa na kundi la chama kinachohusika na Afrika, ambacho kinapata fedha kutoka katika uchumi wa Ujerumani. Lakini kazi hiyo inakuwa ngumu , anasema Asman Nitardy ambaye anashughulika na chama hicho katika eneo la Afrika mashariki. Kutokana na kazi yake amesababisha makampuni mengi kujizuwia kutoa picha mbaya ya Afrika katika vyombo vya habari.
Mwandishi : Maja Braun /ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman