Kenya: Rais Kenyatta atangaza baraza la mawaziri
25 Aprili 2013Matangazo
Hata hivyo jambo linalotarajiwa kuzusha mdahalo mkubwa ni kujumuishwa katika Baraza hilo majina ya wanasiasa wawili maarufu walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita. Majina hayo ni Najib Balala ambaye amependekezwa kuwa madini, wakati Charity Ngilu, akipendekezwa waziri mpya wa nyumba na makaazi. Muda mfupi uliopita nimezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya, Bobby Mkangi, ambaye kwanza alianza kwa kueleza sababu za Rais Kenyatta na naibu wake, William Ruto, kuchukua muda mrefu kulitangaza baraza hilo.
Mwandishi: Bruce Amani
Mhairri: Josephat Charo