1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya, Tanzania na Uganda zaomba kuwa mwenyeji wa AFCON 2027

28 Aprili 2023

Mataifa matatu ya Afrika Mashariki ya Kenya, Uganda na Tanzania yamewasilisha maombi ya kuwa wenyeji wa michuano ya kandanda barani Afrika AFCON mwaka 2027.

Fußball | Africa Cup of Nations | Mosambik - Ruanda
Picha: Muzi Ntombela/BackpagePix/empics/picture alliance

Iwapo yatafanikiwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika kutimua vumbi kwenye eneo la Afrika Mashariki katika kipindi cha miaka 50.

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF  limethibitisha kupokea maombi ya nchi hizo tatu pamoja na maombi kutoka mataifa ya Algeria, Botswana na Misri.

Waziri wa michezo wa Kenya Ababu Namwamba amesema maombi hayo yametumwa bada ya kuamilika majadiliano na wenzake wa Uganda na Tanzania.

Chini ya mpango uliopo mataifa hayo yataunda kamati ya pamoja itakayoratibu kuwania nafasi ya kuwa mwenyeji na maandalizi ya michuano hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW