Kenya, Tanzania zakabiliwa na kimbunga Hidaya
3 Mei 2024Matangazo
Mapema ofisi ya Rais wa Kenya, William Ruto ilitangaza taadhari ya kutokea kimbunga Hidaya, ambacho kitakuwa na upepo mkali na kuathiri zaidi maeneo ya pwani, tangazo ambalo pia limetolewa kwa upande wa Tanzania ambako mvua kubwa na mafuriko vimesababisha watu 155 kupoteza maisha.
Mbali na kupoteza maisha ya watu 188 nchini Kenya tangu Machi, mafuriko hayo yamesababisha watu 165,000 kuyahama makazi yao, huku 90 wakiripotiwa kutojulikana walipo, hali ambayo serikali imewataka raia kuwa na tahadhari.