1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Wadau wasisitiza amani katika uchaguzi Kisumu

Musa Naviye5 Mei 2022

Mashirika ya kutetea amani katika jimbo la Kisumu nchini Kenya yametaka wadau katika kuendelezakudumisha amani, usalama na utulivu kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 2022

Feiertag in Kenia I Mashujaa Day I Symbolbild
Picha: Dai Kurokawa/epa/dpa/picture alliance

Wito huo unakuja ikiwa zimesalia takriban siku tisini kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, uliangalia zaidi katika maeneo ambayo yamekuwa na upinzani mkali wa kisiasa, kutofutwa kwa katiba na miongozo ya uchaguzi iliowekwa kadhalika watu kutopewa nafasi ya kujieleza.

Mwenyekiti Kamati ya Usalama Kisumu ya Kati Antone Okew ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Jukwa la Amani jimbo la Kisumu anasema kinyume na awali, wanatazamia uchaguzi mkuu wenye utulivu wa kiwango cha juu ikizingatiwa siasa za ahadi ya kitaifa.

Hata hivyo, alisema shuguli nzito ingalipo hasa ikizingatiwa siasa za mashinani katika nyadhifa mbalimbali za siasa.

'' tunaona hii amani imekuwa nzuri, ni kutengeneza yale madogo madogo" alitoa athmini yake mwenyekiti huyo wa jukwaa la amani katika jimbo la Kisumu.

Aliongeza Kenya ina historia nzito katika suala la uchaguzi mkuu na hivyo ni muhimu kwa ushirikiano utakaosaidia kudumisha uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia sheria za nchi.

Soma zaidi:Kenyatta amvaa naibu wake Ruto akimtaka ajiuzulu

"Uchaguzi wetu pia huwa na vurugu na sio tu kwa wananchi bali pia kwa taasisi zote.'' alisema huku akirejea hali ilivyokuwa katika baadhi ya chaguzi zilizopita kukumbwa na kadhia ya vurugu na hata baadhi ya watu kuyakimbia makazi yao

Asasi za kiraia zapigilia msumari wito huo.

Asasi za kiraia ambazo zimekuwa zikihudumu moja kwa moja katika ngazi ya jamii zimekuwa zikitekeleza jukumu lake la kuhakikisha inakumbusha mamalaka pamoja na wapiga kura kuhakikisha katiba, sheria na kanuni zinafuatwa katika zoezi hilo la kidemocrasia.

Michael Oyugi washirika la Champions of Peace anasema, ufanisi zaidi wa hatua zilizowekwa kudumisha amani inahitaji ushirikiano wa pamoja wa wadau kutoka muungano wa mashirika ya kijamii, vyombo vya habari, vyombo vya usalama miongoni mwa wadau wengine.

Askari polisi Kenya wakiwa katika majukumu katika uchaguzi mdogo NakuruPicha: Wakio Mbogho/DW

''Kuna umuhimu wa ushirikiano na asasi za usalama ili pawepo mazingira ya usawa"

Soma zaidi:Mchakato wa kumpata mgombea mwenza wa Raila

Kuhusu usalama wa waandishi wa habari kwenye zoezi la uchaguzi mkuu, Katibu wa muungano wa waandishi wa habari Kisumu - Wycliffe Odera alipongeza hatua ya Baraza la Vyombo vya habari nchini Kenya, MCK kuwasaidia waandishi katika mchakato wa zoezi la uchaguzi mkuu huo.

''Kama waandishi wa habari Kisumu, ni msimu wa hatari katika kazi yetu" alisema huku akiwakumbusha wanahabari wajibu wao wakutofuata matakwa ya wanasiasa na kutumika vibaya kwenye matokeo ya kuteteresha amani ya umma

Ujumbe huu wa amani na umoja unajiri hukuzoezi la uchaguzi la mchujo kuwachagua viongozi wa kisiasa watakaopeperusha bendera za vyama vyao likikamilika, zoezi ambalo lilikumbwa na malalamiko miongoni mwa baadhi ya wagombea na wapiga kura. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW