1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Kenya: Watu 5 wafariki katika ajali ya maporomoko ya mgodi

10 Julai 2024

Watu 5 kati ya 18 waliofunikwa na kifusi kwenye maporomoko ya mgodi wa dhahabu jimbo la Migori Magharibi mwa Kenya wamethibitishwa kufariki, hata hivyo ripoti zinaeleza kuwa wengine 14 wameokolewa.

Magari yakiwa kwenye mgodi
Magari yakiwa kwenye mgodiPicha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Hapo jana siku ya jumanne, wachimba migodi takriban 18 walifukiwa na kifusi cha mchanga kwenye mgodi ulioporomoka katika kijiji cha  Kanga, Rongo jimbo la Migori eneo la Nyanza Magharibi mwa Kenya juhudi za uokoaji zikikabiliwa na changamoto ikizingatiwa urefu wa futi 750 wa mgodi huo.

Hata hivyo, juhudi za haraka zilifanikiwa kuwaokoa wachimba migodi 6 wengine zaidi ya 10 wakisalia ndani, Maurice Otieno na Calvin Abich ni baadhi ya wakaazi walioshuhudia na kujitokeza kushiriki harakati za uokoaji.

"Naona wanachangamka, wale watu wanaookoa waathirika waliofunikwa na udogo." Aliiiambia DW mmoja wa wakaazi katika eneo hilo.

Kulingana na naibu kamishna wa jimbo la Migori George Otenga, watu watano wamefariki, watatu wakifariki  mgodini na wengine wawili wakifariki walipokuwa wanatibiwa  katika hospitali ya eneo hilo zoezi ambalo tayari limeng'oa nanga.

"Mkasa huu umeifanya serikali kurejelea mipango ya usalama wa wachimba migodi huku wanaendesha shuguli migodini wakitakiwa kuhakisha wanapata vibali kamili vya kushiriki shughuli migodini." Aliwaambia wakaazi alipotembelea eneo hilo la mkasa.

Aliongeza kwamba "hii ikiwa katika hatua mojawapo ya sheria za serikali zilizowahi kushinikizwa mwaka jana kuangazia usalama migodini nchini Kenya."

Kuimarishwa kwa mikakati ya usalama migodini

Wachimba migodi wanusurika Afrika Kusini

01:27

This browser does not support the video element.

Akihutubia waandishi wa habari, naibu kamishna huyo ameongeza kuwa, serikali itaimarisha mikakati ya usalama ambapo maafisa kutoka mamlaka ya mazingira NEMA wakishirikiana na wenzao kutoka asasi simamizi ya uchimbaji madini na maafisa wa polisi wataendesha oparesheni ya ukaguzi wa migodi kubaini usalama wake, migodi ambayo sio salama ikifungwa.

"Kando na kufunga migoi ambayo sio salama, uwakilishi wa serikali Migori unalenga kuwaelekeza wachimba migodi kuhusu mbinu salama za kuhudumu migodini." Alisema.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW