1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Watu 5 wafariki katika ajali kwenye mgodi wa dhahabu

25 Mei 2024

Watu wasiopungua watano wamekufa na wengine kadhaa haijulikani walipo baada ya maporomoko kushuhudiwa katika mgodi wa dhahabu usio rasmi wa Hillo, kaskazini mwa Kenya.

Watu wakiwa kwenye mgodi wa dhahabu huko Geita, Tanzania
Watu wakiwa kwenye mgodi wa dhahabu huko Geita, TanzaniaPicha: LUIS TATO/AFP

Watu wawili waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu hospitalini. Kamishna wa Kaunti ya Marsabit David Saruni amesema ajali hiyo imesababishwa na  mvua kubwa zilizoshuhudiwa eneo hilo.

Kamishna wa eneo hilo Paul Rotich amesema ripoti kutoka kwa vikosi vya uokoaji, polisi na mamlaka zingine imebainisha kuwa wachimbaji wanane walikuwa ndani ya mgodi huo wakati wa ajali hiyo.

Kituo cha Citizen TV kimeripoti kuwa shughuli za uchimbaji madini ziliendelea licha ya mamlaka kufunga mgodi huo karibu na mpaka wa Ethiopia mnamo mwezi Machi, baada ya watu kadhaa kuuawa kufuatia mapigano kati ya jamii za wenyeji juu ya udhibiti wa eneo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW