Kimbunga Hidaya chasababisha Kenya kuahirisha kufungua shule
3 Mei 2024Rais Ruto amesema kwenye hotuba yake ya hali ya taifa hii leo kwamba ripoti za mamlaka za hali ya hewa zinaibua wasiwasi, huku akikiangazia Kimbunga Hidaya kinachotarajia kuipiga pwani ya Kenya siku zijazo.
Mamlaka za hali ya hewa zimetahadharisha kwamba Kenya itakumbwa na kimbunga cha kwanza kabisa kinachoitwa Hidaya na kusababisha mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makubwa na kuathiri shughuli za baharini na makazi ya eneo la pwani. taifa letu linatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuyakabili maafa na kulinda maisha ya watu na mali.
Kenya, Tanzania zakabiliwa na kimbunga Hidaya
Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki yameelemewa na mafuriko, na sasa zaidi ya watu 150,000 wanaishi kwenye makambi baada ya kulazimika kuyakimbia makaazi yao.