1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaandaa kongamano na mifum ya afya Afrika Mashariki

27 Juni 2023

Kongamano la kwanza la masuala ya kufadhili miradi na mifumo ya afya linawaleta pamoja wadau wa sekta hiyo Afrika Mashariki kujadili jinsi mifumo hiyo inavyoendana na mipango ya kitaifa na kikanda.

Polio in Afrika | Impfstoff in Kenia
Picha: SIMON MAINA/AFP/Getty Images

Mkutano huo wa siku tatu unawaleta pamoja wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, Baraza la Mawaziri, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, mashirika ya Global Fund, Wakfu wa Gates, USAID na UNAIDS.

Kikao kama hiki kiliwahi kufanyika Malawi na Zambia na Kenya ni ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Kwa upande wake, Umoja wa Afrika umezipa wajibu wa kuunga mkono mijadala ya njia bora za kufadhili mifumo ya afya ya nchi wanachama.

Soma zaidi: Mkutano wa ufadhili wa afya wafunguliwa Nairobi

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Kenya, Susan Nakhumicha, mijadala kama hiyo "inatoa fursa ya kuzungumzia na kusaka njia mujarabu za kufadhili mifumo ya afya."

Watu wenye ulemavu wakiwa wamekusanyika kwenye bustani ya NairobiPicha: DW

Kwenye kongamano hilo, wataalamu wanawasilisha hoja na maelezo ya utafiti kuhusu njia mwafaka za kufadhili mifumo ya afya zitakazowaelimisha watunga sera na kuwawezesha kupambana na changamoto zinazozikabili nchi.

Njia za kupambana na changamoto za afya

Kwa upande wake, serikali ya Kenya inanuwia kujikita kwenye mbinu za kuzuwia magonjwa kwa kufuata kanuni za afya badala ya kusubiria matibabu pale mtu anapougua.

Kikao hicho cha kikanda kinafanyika wakati ambapo sekta ya afya nchini Kenya imetengewa shilingi bilioni 141.2 katika bajeti ya mwaka 2023/24.

Hiki ni kiwango ambacho kimepungua kwa shilingi bilioni 5.6, kwani bajeti iliyopita sekta ya afya ilitengewa shilingi bilioni 146.8, kwa mujibu wa Anne Waiguru, mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Kenya.

Picha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Mkutano huu wa kilele utawapa fursa wadau na baraza la magavana kuwasilisha mapendekezo kadha wa kadha zikiwemo pia njia za kuimarisha utoaji huduma kutoka kwa hazina ya Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) na pia kuzindua mifumo mingine ya ufadhili kwa madaraja tofauti ya vituo vya afya nchini,  zinaeleza duru rasmi.

Akiwa kwenye hafla nyengine, Rais William Ruto aliwaahidi madereva wa pikipiki za umma maarufu bodaboda kwamba watajumuishwa kwenye mfumo wa NHIF.

Imetayarishwa na Thelma Mwadzaya/DW Nairobi

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW