1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaimarisha usalama ikihofia maandamano mapya

27 Juni 2024

Polisi nchini Kenya wameweka vizuizi vya barabarani kwenye mitaa inayoelekea kwenye makaazi ya rais siku ya Alhamisi.

Kenya : Maandamano Nairobi
Kumeshuhudiwa maandamano na mahali pengine utulivu siku ya Alhamisi.Picha: Daniel Irungu/EPA

Hayo yanafanyika wakati waandamanaji wakisisitiza kuyavamia na kuyakalia makaazi hayo, licha ya Rais William Ruto kutangaza kuuondosha muswada wa fedha unaozozaniwa wa mwaka 2024, uliochochea maandamano makubwa.

Haikuwa wazi ni kwa umbali gani waandamanaji hao wangeridhishwa na uamuzi huo wa Rais Ruto, Jumatano siku moja baada ya machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 23 na kushuhudia bunge likivamiwa.

Kumeshuhudiwa maandamano na mahali pengine utulivu siku ya Alhamisi nchini humo na hakukuwa na purukushani kama zilizoshuhudiwa huko nyuma.

Ruto anakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi katika kipindi cha utawala wake wa miaka miwili, wakati wasiwasi ukizidi kufuatia maandamano yanayoongozwa na vijana kutokana na shutuma za ongezeko la kodi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW