1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaipa Adani group mkataba wa kujenga nguzo za umeme

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Kampuni ya Adani Group ya India na Africa50, ambalo ni tawi la benki ya Maendeleo ya Afrika linalosimamia miundombinu, zimepewa na serikali ya Kenya, mkataba wa kujenga nguzo mpya za umeme.

Kenya
Kampuni ya Adani Group na Africa50 zimepewa mkataba wa kujenga nguzo za umeme na serikali ya KenyaPicha: Michael Gottschalk/photothek/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa mshauri wa uchumi wa Rais William Ruto, David Ndii. Kupitia jukwaa la X, Ndii amesema mkataba huo una thamani ya dola bilioni 1.3 na kwamba tayari makampuni hayo yameanza kuajiri watakaohusika kuutekeleza mradi huo.

Soma zaidi: Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya wagoma

Hivi karibuni, mpango mwingine wa serikali ya Kenya wa kuukodisha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata kwa kampuni ya Adani Group kwa miaka 30 ,ili ifanye uwekezaji wa dola za Kimarekani bilioni1.85 uliibua hasira kali miongoni mwa Wakenya.

Hali hiyo ilisababisha wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga nchini humo kufanya mgomo.