1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yajitahidi kuboresha miundombinu ya walemavu

8 Novemba 2024

Watu wenye ulemavu katika mataifa mengi ya kimasikini, wana wakati mgumu sana panapohusika usafiri wa kuwatoa mahala pamoja kuwapeleka pengine, kwani miundombinu na vyombo vya usafiri wa umma si rafiki kwao.

Bungui I Rollstuhlbasketballer
Picha: Florent Vergnes/AFP

Caroline Mwikali alipoteza uwezo wake wa kutembea akiwa na umri wa miaka 13 baada ya kuuguwa kwa muda mrefu. Haraka mno akajifunza kwa jinsi gani ni vigumu kutembea kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi.Watanzania wenye ulemavu wataka kanuni za wazi kuwahusu

Mwikali, ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye kampuni ya ufadhili wa magari, anasema usafiri wa umma haukubuniwa kuwafaa watumiaji walemavu kama yeye.

Usafiri mashuhuri wa Nairobi unajumisha bodaboda, matatu na tukutuku, ambazo zote hazina vifaa maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Kwenye mabasi yaitwayo matatu, kwa mfano, hakuna hata nafasi ya kuweka viti vya maringi matatu vinavyotumiwa na watu wenye ulemavu na badala yake abiria wa aina hiyo huwekwa kwenye viti vya kawaida na vigari vyao vya maringi matatu kuswekwa kwenye eneo la mizigo.

Mashindano ya mbio za watu wenye ulemavu wanaotembelea kiti cha magurudumu KenyaPicha: Frederik Lernryd/AFP/Getty Images

Mwikali anasema na hapa namnukuu: "Mara nyingi, watu wanaofanya kazi kwenye vituo vya mabasi wanapaswa kukutowa kwenye kiti cha maringi matatu na kukusaidia kupanda kwenye basi. Hili sio tu kwamba halipendezi lakini linakufanya uwape watu nafasi ya kukuangalia sana bila sababu." Mwisho wa kumnukuu.

Walemavu wa kusikia kujitokeza kupiga kura SenegalMwanamke huyu ni sehemu ya asilimia 2.2 ya Wakenya, ama watu 900,000, wanaoishi na ulemavu. Sehemu kubwa ya watu hao ni wale wasiokuwa na uwezo wa kutembea, ambao ni asilimia 42 ya watu wote wenye ulemavu.

Mjasiriamali mmoja, Daniel Gatura, alianzisha kampuni ya Ace Mobility jijini Nairobi mnamo mwaka 2021. Vyombo vya usafiri kwenye kampuni hii vimebuniwa upya ili kuweka viti na vifaa vya kuwawezesha watu wenye uonevu na mwengine yeyote anayehitaji msaada wakati wa usafiri.

Jinsi kampuni ya mpira inaboresha maisha ya walemavu Kenya

01:35

This browser does not support the video element.

Gatura anasema kilichomfanya aanzishe kampuni hii ni uzoefu wake binafsi akiwa mdogo. Baba yake alipata ajali mbaya na akavunjika uti wa mgongo na matokeo yake akawa mlemavu anayetumia kigari cha magari matatu maishani mwake mote.

Wakati huo, Gatura alikuwa na miaka mitano tu, na akashuhudia jinsi mzazi wake huyo alivyokabiliana na changamoto kadhaa, ikiwemo ya kupoteza ajira kutokana na ugumu wa kusafiri.Kiwakumbacho walemavu wa ngozi si mauaji pekee

Kupitia kampuni ya Gatura ya Ace Mobility, watumiaji wanaweza kuagizia chombo cha usafiri kupitia programu kwenye simu yake. Madereva wamefunzwa kuwa watoa huduma, wakihakikisha kwamba wanafahamu jinsi ya kutoa msaada kwa adabu na heshima kwa abiria wenye kuishi na ulemavu.

Hadi sasa, kuna watumiaji 5,000 wa huduma hiyo jijini Nairobi. Gatura anasema na hapa namnukuu: "Tunabadilisha stori kuhusu ulemavu na kupunguza gharama na shida za kutembea. Kuwa na ulemavu hakumaanisha kwamba huwezi kujitafutia riziki, haimaanishi kwamba huna thamani kwenye jamii." Mwisho wa kumnukuu.

Wanawake wenye ulemavu wajiunga na mchezo wa mpira wa mikono

03:51

This browser does not support the video element.

Lakini tatizo moja lipo wazi. Usafiri huu maalum ni ghali zaidi kuliko ule wa umma, kwani kila kilomita moja, kampuni hii hutoza dola moja ya Kimarekani, kiwango ambacho kinaweza kutumika kulipia hadi masafa ya kilomita 40 kwenye usafiri wa umma.

Raha na wepesi wake ni kwamba usafiri huu huwafikisha watu wenye ulemavu na dhiki nyengine za kimaumbile - kama vile wagonjwa - moja kwa moja mahala wanakotaka wapelekwe.Fred Batale na juhudi za kuwasaidia walemavu wenzake

Kwa wasafiri kama Mwikali tuliyeanza naye hapo awali, Ace Mobility ni njia nyepesi na rahisi zaidi ya kusafiri na kufika watakako. Anasema binti huyu, "naweza kusafiri kwa raha na vila ya kulazimika kuondoka kwenye kiti changu cha maringi matatu, na pia heshima yangu inalindwa."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW