1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yajiweka sawa dhidi ya Ebola

Wakio Mbogo28 Septemba 2022

Wizara ya afya nchini Kenya imetangaza kaunti 20 kati ya kaunti 47 kuwa maeneo yaliyo kwenye hatari zaidi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, wakati huu taifa jirani la Uganda linashuhudia mlipuko wa ugonjwa huo.

Kongo Beni Ebola-Opfer
Picha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Wizara ya afya nchini Kenya imetangaza kaunti 20 kuwa maeneo yaliyo kwenye hatari zaidi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, wakati huu taifa jirani la Uganda linashuhudia mlipuko wa ugonjwa huo.

 Kenya imesema tayari inaweka mikakati inayohitajika ikiwemo kuwachunguza wasafiri na kuunda vituo vya kuwatenga wagonjwa, ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo. Mwandishi wetu Wakio Mbogho anasimulia zaidi.

Wizara ya afya ya Kenya imeunda mpango wa dharura utakaotoa mwongozo wa namna ya kuzuia na kupambana na virusi vya Ebola nchini.

Serikali imeunda jopokazi la pamoja kuhusu ugonjwa wa Ebola, lililotwikwa jukumu la kutambua dalili za hatari, kufanya tathmini ya mara kwa mara, na pia kuimarisha uchunguzi wa watu katika maeneo ya mipaka ya nchi.

Soma pia:Kenya yatangaza tahadhari ya Ebola Busia

 Kaimu mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya daktari Patrick Amoth kutokana na taifa hilo kuwa na muingiliano mkubwa na Uganda kuna haja ya kuchukua tahadhari hasa katika maeneo ambayo yanamuingiliano mkubwa, kijamii, kibiashara na hata kitamaduni.

"Kwa hiyo tunapozingatia kitisho hicho, tunatekeleza hatua za ufanisi kuhakikisha, kwanza, tunazuia mlipuko huo kuvuka mipaka." Alisema kaimu mkurugenzi mkuu wizara ya afya daktari Patrick.

Aliongeza kuwa iwapo ugonjwa huo utaingia, kutokana na muingiliano mkubwa uliopomamlaka hiyo imejiweka tayari katika kukabiliana na udhibiti wa maambukizi hayo ya homa hatari.

Wiki moja baada ya taifa la Uganda kutangaza kisa cha kwanza cha kifo cha mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya Ebola, matukio ya vifo yameongezeka kwa kasi, vifo 23 vikiripotiwa kufikia sasa.

Kaunti 20 kati ya 47 zipo kwenye hatari zaidi

Wiki moja baada ya taifa la Uganda kutangaza kisa cha kwanza cha kifo cha mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya Ebola, matukio ya vifo yameongezeka kwa kasi, vifo 23 vikiripotiwa kufikia sasa.

Hali ya Ebola Uganda

Wizara ya afya ya Kenya imetangaza kuwa kaunti 20 kati ya 47 ziko kwenye hatari ya maambukizi. Busia ambao ni mji ulio mpakani unaongoza kwenye orodha hii kutokana na biashara na shughuli za uchukuzi kati ya mataifa haya mawili.

Soma pia:DRC: Yazindua kampeni ya chanjo ya Ebola

Mji huo unafuatiwa na kaunti ya Nakuru iliyosheheni bandari kavu eneo la Naivasha, inayohudumia ukanda wa kaskazini na kuunganisha Kenya na mataifa ya Afrika mashariki. Kaunti zingine zilizotajwa kuwa hatarini ni pamoja na Kiambu, Nairobi, Kajiado, Machakos, Taita Taveta na Mombasa.

"Ukanda wote kutoka maeneo yanayopakana na Uganda, kutoka Turkana Kaskazini Magharibi hadi Migori Kusini Magharibi."

 Taarifa ya wizara hiyo ilisema na kuongeza kwamba maeneo yote ya barabara kuu kutoka Busia hadi Mombasa, maeneo yote hayo yako hatarini na huenda hapo ndipo kisa cha cha kwanza kikapatikana kutoka katika ukanda huo.

Wakaazi wa mipakani watahadharishwa

Wakati wizara ya masuala ya afya katika taifa hilo la Afrika mashariki ikiendelea kuchukua jitihada za kudhibiti maambukizi yasifike katika nchi hiyo, imetoa hamasa miongoni mwa jamii kutambua kuhusu virusi hivi vya Ebola.

Mbali na kuitambua wataalamu wa masuala ya afya wameendelea kutoa elimu namna vinavyoambukizwa, dalili za ugonjwa, njia ya kujiepusha au hata mahali ambapo mtu anaweza kupata usaidizi.

DR Kongo yaripoti maambukizi mapya ya Ebola

01:09

This browser does not support the video element.

Wananchi wanaoishi karibu na mpaka wa Kenya na Uganda wametahadharishwa kuripoti mara moja wanaposhuhudia mgeni yeyote akiingia nchini kwa kupitia njia za vichochoro.

Soma pia:Tedros mgombea pekee WHO licha ya kupingwa na Ethiopia

Gavana wa TansNzoia George Natembeya amewahimiza wakaazi kuchukua jukumu la kibinafsi kwa kushirikiana na mamalaka katika kutoa taarifa ya watu ambao wanaingia nchini kienyeji ili hatua za udhibiti zichukuliwe.

Wizara ya afya vilevile imetoa hakikisho kwamba inafanya maandalizi kuwawezesha wote watakaokuwa wanawashughulikia wagonjwa wana vifaa vinavyohitajika kwa wakati unaofaa, ili kuyalinda maisha ya maafisa wa afya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW