1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yakabiliwa na uhaba wa chanjo muhimu kwa watoto

30 Mei 2024

Wazazi nchini Kenya wanakabiliana na uhaba wa chanjo za msingi katika hospitali za umma, baadhi ya hospitali hazina dozi zozote na huku miongoni mwa chanjo hizo ni pamoja na magonjwa ya Pepopunda na Kifua kikuu.

Mhudumu wa afya akiwa akionesha chanjo ya kipindupindu
Mhudumu wa afya akiwa akionesha chanjo ya kipindupinduPicha: JEKESAI NJIKIZANA/AFP/Getty Images

Uhaba mkubwa wa chanjo za msingi umeziandama hospitali za umma kote nchini na kuwaacha watoto wachanga, kina mama wajawazito na wengine walio na matatizo ya afya hatarini. Katika kaunti ya Baringo, hospitali za umma hazina dozi mpya baada ya kusambaza shehena yake ya mwisho.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa afya wa kaunti ya Baringo Solomon Sirma, dozi zote zimekwisha baada ya kuzigawa kwa hospitali za Mogotio, Eldama Ravine, Tiaty na sehemu zote za Baringo.

Betsy Toroitich ana mtoto wa miezi mitano na amelazimika kusafiri hadi hospitali ya rufaa ya Baringo ili kuhakikisha mtoto wake anapata chanjo muhimu , lakini ameambulia patupu.

Soma pia:Uganda imeanza kapemini ya kutowa chanjo ya homa ya manjano nchi nzima

Kwenye barua yake ya katikati ya mwezi huu huu wa Mei kwa waziri wa afya wa Kenya Susan Nakhumicha, baraza la magavana lilitoa tahadhari kuhusu uhaba wa chanjo kwenye kaunti zote 47 kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Chanjo hizo zilizo haba ni za BCG ya Kifua kikuu, OPV/IPV ya Kupooza, MR ya ukambi, Pepopunda na Rota Virus. Eneo la pwani limesitisha utoaji wa chanjo kwenye hospitali za umma kwani hakuna dozi.

Huko Mlima Kenya baadhi ya wazazi wamelazimika kutafuta chanjo kwenye hospitali jirani za eneo hilo. Kwa kaunti ya Nairobi dozi zilizopo hazifiki nusu ya kiwango kinachohitajika alese,a Tom Nyakaba, afisa mkuu wa afya wa serikali.

Serikali yakiri uhaba mkubwa wa chanjo

Kwa upande wake, wizara ya afya ya Kenya katika taarifa yake iliyotiwa saini na katibu wa kudumu wa huduma za afya Harry Kimtai, inasema mikakati ipo ya kukabiliana na uhaba huo wa chanjo.

Utoaji chanjo ya Malaria washika kasi Cameroon

02:11

This browser does not support the video element.

Wizara ya afya imekiri kuwa upo uhaba wa kitaifa ila inajitahidi kuiongeza kasi ya chanjo zilizolipiwa kuwasili nchini kuwasili katika wiki za mwanzo za mwezi ujao wa Juni kutokea shirika la Umoja wa Matifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Soma pia:WHO yatahadharisha juu ya uhaba wa chanjo ya kipindupindu

Kadhalika wizara ya afya imetengewa shilingi bilioni 1.25 kwenye bajeti ya kugharamia chanjo za msingi ijapokuwa kiwango hicho ni nusu ya kile cha awali. 

Wakati huo huo, mipango ipo ya kuanza kutengeneza chanjo za binadamu ifikapo mwaka 2027 baada ya Benki ya Dunia kutoa ufadhili wa dharura wa dola bilioni za Marekani kwa mataifa 8 ya Afrika. Kenya tayari imeanza ujenzi wa kituo hicho kwenye kiwanda chake cha Biovax mtaani Industrial Area.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW