1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Kenya yamkamata mshukiwa wa mauaji ya makumi ya watu

15 Julai 2024

Polisi ya Kenya imetangaza leo Jumatatu, imemkamata mshukiwa wa mauaji ya kupanga baada ya kugundulika miili ya watu tisa iliyokatwakatwa vipande na kutupwa katika dampo la kutupa taka mjini Nairobi.

Kisa cha kupatikana miili ya watu Kenya
Miili ya watu iliyopatikana imetupwa ikiondolewa na maafisa wa usalama na wananchi Kenya.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Mkurugenzi wa kitengo cha kuchunguza matukio ya uhalifu Mohammed Amin amewaambia waandishi habari kwamba mshukiwa mkuu wa tukio hilo la kutisha alikamatwa leo asubuhi.

Amemtaja mshukiwa huyo kama muuaji anayepanga kuwaua watu na mbaye hajali uhai wa binadamu. Polisi imesema mshukiwa huyo amekiri kuwauwa wanawake 42.

Kaimu Mkuu wa jeshi la polisi la Kenya Douglas Kanja amesema kuwa miili sita ya kwanza ilipatikana Ijumaa, na miili mingine ilipatikana jana Jumamosi. Kanja ametoa wito kwa wananchi kuonesha ushirikiano ili kufanikisha kuwapata wahusika wa unyama huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW