1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Kenya yamrejesha anayedaiwa kumuua mpenzi wake Marekani

2 Septemba 2024

Waendesha mashitaka wa Kenya wamesema leo kwamba wamemrudisha Kevin Kang'ethe anayeshitakiwa kwa kumuua mpenzi wake nchini Marekani, katika kesi iliyogonga vichwa vya habari baada ya kutoroka mahabusu jijini Nairobi.

Mahakama ya juu ya Kenya
Mahakama ya juu ya KenyaPicha: Tony Karumba/AFP

Waendesha mashitaka wa Kenya wamesema leo kwamba wamemrudisha Kevin Kang'ethe anayeshitakiwa kwa kumuua mpenzi wake nchini Marekani, katika kesi iliyogonga vichwa vya habari baada ya kutoroka mahabusu jijini Nairobi.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma imesema katika taarifa kwamba Kang'ethe aliondoka Kenya jana Jumapili na atakabiliwa na shtaka la mauaji katika mahakama moja mjini Boston siku ya Jumanne.

Soma pia: Polisi Kenya yatangaza zawadi kwa muuaji alietoroka

Kang'ethe alikamatwa tena mwezi Februari akiwa amejificha nyumbani kwa jamaa zake jijini Nairobi. 

Mshitakiwa huyo alikimbia Marekani baada ya kumuua, Margareth Mbitu, ambaye mwili wake ulikutwa kwenye maegesho ya magari kwenye uwanja wa ndege wa Boston mwezi Novemba. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW