1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Kenya yamzika Mkuu wa Majeshi aliyekufa kwa ajali

21 Aprili 2024

Mkuu wa Majeshi ya Kenya, Jenerali Francis Omondi Ogolla amezikwa hii leo nyumbani kwake Ng'iya, Kaunti ya Siaya magharibi mwa Kenya siku tatu tangu alipoaga dunia kutokana na ajili ya helikopta ya jeshi.

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla.
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla.Picha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Rais William Ruto aliwaongoza waombolezaji wakiwemo viongozi wa serikali na wanasiasa katika tukio hilo lililoendeshwa kwa taratibu za kijeshi. Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Dotto Biteko alimuwakilisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Jenerali Ogolla na maafisa wengine tisa wa jeshi walifariki dunia Alhamisi wiki hii wakati helikopta yao ilipoanguka katika eneo la misitu la Sindar, katika Kaunti ya Elgeyo Markweti kaskazini magharibi mwa Kenya.

Maafisa wawili wa kijeshi walinusurika katika ajali hiyo. Jenerali Ogola alikuwa na umri wa miaka 62 na amemuwacha mjane na watoto wawili.

Alikuwa amewatembelea wanajeshi wanaoendesha operesheni ya usalama katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa, ambalo limekumbwa na uhalifu unaofanywa na wavamizi na wezi wa mifugo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW