1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yarekodi kisa cha kwanza cha maradhi ya mpox

30 Agosti 2024

Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha mpox katika mji wake mkuu, Nairobi, kutoka kwa mgonjwa mmoja anayezuiwa karantini na kufanya visa jumla kufikia vitatu, imesema Wizara ya Afya imesema hii leo.

Mshukiwa wa Mpox akichukuliwa vipimo.
Mshukiwa wa Mpox akichukuliwa vipimo.Picha: Xinhua/IMAGO

Mgonjwa huyo aliingia Kenya wiki iliyopita akitokea Uganda, amesema Mkurugenzi Mkuu wa afya Patrick Amoth kwenye taarifa yake na kuongeza kuwa alikuwa ametengwa kwenye hospitali ya Nairobi na hali yake inaimarika.

Hicho ni kisa cha kwanza cha ugonjwa huo jijini Nairobi, lenye wakazi milioni 4.4 kulingana na sensa ya karibuni ya 2019.

Soma pia:Ufadhili wa mapambano ya Mpox Afrika wachechemea

Hayo yanatokea wakati, Shirika la Afya ulimwenguni likisema chanjo ya mpox itawasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kulikoanzia maradhi hayo, siku chache zijazo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW