Kenya yatafuta amani miaka 60 baada ya uhuru
15 Septemba 2026
Sanamu ya mpigania uhuru mashuhuri Dedan Kimathini vigumu kukosa kuiona kwa mtu yeyote anayetembea katikati ya Nairobi, mji mkuu wa Kenya kama urathi wa historia ya Kenya na harakati zake za kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni wake wa Uingereza.
Taifa hilo lilipata mwanzo mpya wakati Prince Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, alipokabidhi rasmi mamlaka mnamo Desemba 12, 1963, baadaye ikajulikana kama Jamhuri Day — "Siku ya Jamhuri."
Soma pia:Kenya yatumbukia gizani kwa mara ya tatu ndani ya miezi mitatu
Miaka sitini imepita, sio kila mtu yuko katika hali ya kusherehekea. Berline Ndolo, mwanzilishi na meneja programu ya Mtandao wa Dunia ya Mabadiliko Endelevu (WONESU), shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu Kisumu Magharibi mwa Kenya ambalo linasaidia watu walio katika mazingira magumu katika elimu na kilimo. Katika jukumu zake, anawasiliana kila siku na watu "maskini zaidi ya maskini."
"Kundi hili la watu haliwezi kuwa na furaha siku ya Jamhuri. Kwa sababu ya gharama kubwa ya maisha hivi sasa, ambapo maisha yamekuwa ghali sana kwao, hawawezi kumudu milo mitatu kwa siku, labda hata miwili," Ndolo aliiambia DW.
"Badala yake watazingatia jinsi wanavyoweza kulisha familia zao kwa rasilimali chache walizonazo."
"Gharama ya juu ya maisha" ni msemo wa kawaida kote nchini Kenya siku hizi. Huku Rais William Ruto, sasa akiwa madarakani kwa mwaka mmoja, akipunguza ruzuku na kuanzisha ushuru mpya, hali imekuwa mbaya zaidi.
"Rais alikuwa na ajenda ya ahadi njema kwa watu wa Kenya," Ndolo alisema. "Watu waliompigia kura walikuwa na matumaini makubwa."
Lakini Sasa, anasema, hakuna kinachoonekana kubadilika. "Ikiwa kuna chochote, biashara zinafungwa, watu ambao wako kwenye ajira wanatozwa ushuru mwingi, na bado, tunajitahidi kupata riziki."
Jinsi Kenya ilivyokabiliana na mgawanyiko wa kikabila
Historia ya hivi majuzi ya Kenya imefafanuliwa na mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2007 na mapema 2008. Ushindi mdogo uliopingwa wa Mwai Kibaki, kutoka kabila la Kikuyu, dhidi ya Raila Odinga, ambaye ni Mjaluo, ulizua mapigano makali yaliyosababisha vifo vya hadi watu 1,500. Peter Muchiri, 26, ambaye anafanya kazi katika hoteli moja katika mji wa Nyahururu katikati mwa Kenya, anaelezea mzozo huo kama mwamko kwa taifa.
Soma pia: ICC yasitisha uchunguzi machafuko baada ya uchaguzi Kenya
"Mzozo huo ndio ulikuwa hatua ya mabadiliko," Muchiri alisema. "Kulikuwa na miji na maeneo ambayo huwezi kwenda kutafuta kazi au kuomba msaada kwa sababu kama wewe sio mmoja wao, hakuna anayekujali."
Muchiri alikuwa na umri wa miaka 11 vurugu zilipozuka, Nyahururu ilikuwa mojawapo ya miji iliyochukuliwa kuwa salama wakati huo.
"Nchi ilikuwa katika machafuko makubwa," Muchiri alisema. "Watu walijifunza mengi kutokana na hilo."
Anahisi migawanyiko ya kikabila imepungua tangu wakati huo. "Haijalishi wewe ni wa kabila gani. "Bali wewe ni Mkenya."
James Shikwati, mwanzilishi wa Inter Region Economic Network, anahoji kuwa Rais Ruto amefanikiwa tu kwa kufanya kampeni isiyotegemea kwa kiasi kikubwa jamii ya kikabila.
Alipokuwa akifanya kampeni mwaka wa 2022, Ruto alijifanya "mchuuzi" ambaye alitatizika kutafuta riziki, aliwahurumia maskini na kuahidi kuwaondoa kutoka kwa umaskini.
"Kwa kuunda kabila jipya la 'hustler', kumaanisha watu wa kipato cha chini, tukitumia neno jepesi kama hilo, nadhani alifanya kazi nzuri katika hilo." Kwa kufanya hivyo, Ruto aliwahamasisha Wakenya kufikiria upya muelekeo wa nchi yao, Shikwati alisema.
Kenya sasa inamshutumu Ruto
Kulingana na Shikwati, hii pia ilimaanisha mabadiliko makubwa katika jinsi Wakenya sasa wanavyoutazama urais wa Ruto. "Anachunguzwa kwa ukali," lakini si kwa mtazamo wa kikabila.
"Hawamtaji kwa jina la kabila lake," alisema. "Wanaangazia uchumi tu. Wanasema haufanyi vizuri, watu wanapoteza kazi, makampuni yanafungwa."
Wakati sera za Ruto ziliposababisha bei kupanda, Wakenya wengi waliandamana. Maandamano hayo makubwa ambayo wakati mwingine yaliibua vurugu yalichochewa na Raila Odinga, waziri mkuu wa zamani wa Kenya ambaye alikataa kukubali kushindwa kwake baada ya kushika nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa 2022. Maandamano hayo yamekwisha, lakini ugumu wa uchumi bado uko pale.
Samir Hassan ni baba wa watoto wanne na dereva huko Mombasa, jiji la pili kwa ukubwa nchini Kenya. Ratiba yake mara kwa mara inampeleka kwenye kingo za magharibi mwa jiji ambapo Reli inaunganisha pwani ya Kenya na mji mkuu. Treni hiyo iliyojengwa na China inawapeleka watalii mara tatu kwa siku, lakini kutokana na wengi kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi, watalii hawafiki tena.
"Sasa kila Mkenya anapunguza gharama," Hassan aliiambia DW. "Kwa kawaida, mwezi wa Disemba huwa tuna shughuli nyingi sana kwa sababu ni pwani ni mahali ambapo watu wanapumzika na ndipo tunapata wateja mchanganyiko: wageni na watalii wetu wa ndani.
Miradi mikubwa na madeni yanayoongezeka
Takriban majengo matano kutoka kwenye sanamu ya Dedan Kimathi kuna bustani ya Uhuru, Eneo la kihistoria magharibi mwa Barabara ya Nairobi Expressway ambalo lilikuwa eneo la mapigano ya demokrasia katika miaka ya 1990.
Barabara ya Nairobi Expressway, barabara kuu ya mji mkuu, Inaunganisha katikati ya jiji na uwanja wa ndege na kituo cha reli ya SGR cha Nairobi. Reli ya SGR inaweza kukupeleka Mombasa kwa saa tano, ilizinduliwa mwaka wa 2017, huku barabara ya mwendokasi ya Nairobi ikifunguliwa rasmi mwaka jana.
Soma pia: Raila odinga apanga mikutano zaidi ya hadhara Kenya
Miradi hiyo miwili muhimu ya miundombinu iligharimu mabilioni, na kulingana na mwanauchumi Shikwati, inachangia mengi katika ugumu wa maisha ambao Wakenya wanapitia siku hizi.
Matukio ya sasa yote yanarejea nyuma katika mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2007. Wote wawili, Ruto na Uhuru Kenyatta, mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya, walishtakiwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa majukumu yao katika mgogoro huo. Ili kuepuka kile walichokiita haki ya "kikoloni", waliungana kugombea urais mwaka wa 2012 - na kushinda, huku Kenyatta akiwa rais na Ruto akawa makamu wake.
Uchumi wa Kenya
Ilianza na msururu wa mikopo na mlima unaokua kwa kasi wa madeni. Kulingana na Shikwati, upendeleo katika mfumo wa fedha wa kimataifa na maamuzi potofu ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa pia ulitekeleza wajibu wao. Lakini maamuzi ya Ruto kama rais, kusitisha ruzuku na kuanzisha ushuru mpya, kwa hakika haukufanya mzozo wa kifedha kuimarika.
Kutoza ushuru wa juu kwa uchumi ambao hauna mazao umewacha watu na maamuzi madogo ikiwa ni pamoja na kupunguza shughuli na kufunga makampuni, hatua inayoweka shinikizo zaidi kwa watu.
Soma pia: Upinzani wa Kenya waishutumu serikali kwa kuchochea matabaka
Miaka 60 baada ya uhuru, ubaguzi wa kikabila sio sababu utambulisho wa Kenya. Sasa, ni matatizo ya kiuchumi ambayo yanaweka changamoto katika mustakabali wa nchi.