1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yatangaza sikukuu ya kupanda miti

7 Novemba 2023

Serikali ya Kenya imewashangaza wengi kwa kutangaza sikukuu ya umma ifikapo Novemba 13 kama siku maalum ya upandaji miti kote nchini humo.

Thuku Kariuku  Eco Afrika DW Nairobi Kenya
Mwandishi wa DW Thuku Kariaku akishikilia mchePicha: Thuku Kariuku/DW

Hii ni sehemu ya mpango wake kabambe wa kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2032. 

Hayo yametangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki kufuatia kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika wiki iliyopita na kuongozwa na Rais William Ruto.

Kindiki amesema wananchi wanatarajiwa kupanda miti kote nchini Kenya kama mchango wao wa kizalendo kwa taifa ili kuungana na juhudi za taifa hilo za kupambana na athari mbaya za mabadiliko ya Hali ya Hewa, kama ukame na mafuriko, ambayo yamekuwa yakishuhudiwa eneo la Pembe ya Afrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW