Kenya yatoa zabuni ya ujenzi wa uwanja mpya wa ndege
4 Machi 2026
Matangazo
Katika taarifa jana jioni, Chirchir alisema kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini humo, ilitoa zabuni ya kujenga uwanja mpya wa ndege karibu na JKIA, na kuboresha maeneo ya uwanja uliopo.
Zabuni hiyo ni kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha kushughulikia abiria milioni 10 kila mwaka pamoja na kutengeneza njia mpya za kuruka kwa ndege miongoni mwa mambo mengine.
Mnamo mwezi Novemba 2024, Rais wa Kenya William Ruto aliagiza kufutiliwa mbali kwa mchakato wa ununuzi ambao ungewezesha kampuni moja ya India kwa jina Adani Group kudhibiti uwanja huo wa ndege wa JKIA kufuatia kufunguliwa mashitaka kwa mwanzilishi wake, Gautam Adani, nchini Marekani.