1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
ImaniKenya

Kenya yasherehekea Eid ul Fitr kwa kuombea amani

20 Machi 2026

Waislamu ulimwenguni wanaadhimisha kukamilika wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwa sherehe ya Eid UL Fitr, huku ujumbe wa amani katika migogoro ya vita duniani ikishamiri miongoni mwa viongozi wa kidini na waumini hao.

Kenya Nairobi | Swala ya Eid
Waumini wa dini ya Kiislamu nchini Kenya wamesisitiza amani ulimwenguni wanapoadhimisha sikukuu ya Eid Ul FitrPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Mbali ya kutakiana neema na baraka za sikukuu hii, waumini walipongezana kwa kukamilisha mfungo wa Ramadhan na kuhimizana kuwakumbuka wengine katika jamii kipindi hiki cha sherehe hasa walio katika mazingira magumu baadhi wakielezea utofauti wa mitindo ya jinsi hali zilivyobailika katika kukirimiana.

Suleiman Mohamed ni miongoni mwa waumini hao amesema "Kuhimiza, binadamu warudi kwa ule usawa wa zamani, kuwa na utu, jirani hata kama sio Muislamu una upendo naye sana yani lakini dunia ya sahii sijui tunaelekea wapi, ukiangalia sahii huko Gaza, tusiende mbali hapa tu Sudan baina ya Wao kwa wao wanapigana."

Sudan ni moja ya mataifa yaliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinaadamuPicha: Marwan Ali/AP Photo/picture alliance

Kilele cha Swala ya Eidni hotuba kwa waumini, mashekhe kutoka maeneo mbali mbali ikiwemo Kisumu na Nairobi wakitumia majukwaa yao kukumbuka wahanga wa vita vinavyoendelea katika sehemu mbali mbali za ulimwengu.

Umma waomba kuendeleza matendo mema

Kadhalika, wamehimiza umma kuendelea na utekelezaji wa amali njema ikiwemo kuendekeza ibada ya swala, kusoma Quran na kufanya kheir, msisitizo wa, waishi walivyokuwa kwenye Ramadhani.

Wapalestina waanza kuhama kuelekea kusini mwa Gaza

01:25

This browser does not support the video element.

Sheikh Adan Kala wa msikiti wa Jamia Kisumu na Sheikh Jamaludeen Osman wa msikiti wa Jamia Nairobi amesema "Hakuna neema kubwa kama neema ya Amani, hakuna neema kubwa kama neema ya Afya, ya rizki na watoto na mali hakuna neema kubwa kama Mwenyezi MUNGU kukuepusha na balaa za duniani leo ni siku ya furaha, leo ni siku ya kheir, bila kuwasahau ndugu zetu waliokosa neema ya amani tuwakumbuke kwa dua."

Ibada ya funga kwa waumini wa dini hii, inakamilika huku wenzao waumini wa dini ya Kikristo wakiendelea na mfungo wa Kwaresma itakayokamilika kwa maadhimisho ya Pasaka, mfungo unaojumuisha jumla ya siku 40 huku mfungo wa Kiislamu ukijumuisha mfululizo wa siku 30.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW