Kenya yawarudisha wakimbizi wa Uturuki makwao
22 Oktoba 2024Matangazo
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,UNHCR, limesema hayo kwa shirika la habari la AFP kuwa limesikitishwa sana na hatua hiyo ya Kenya kuwatimua wakimbizi hao. Shirika lingine la Amnesty International nalo limeelezea tukio hilo kwamba linakiuka haki za binadamu na kuondoa uaminifu wa waomba hifadhi nchiniKenya. Hata hivyo, Wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema imechukua hatua hiyo baada ya kupokea hakikisho kutoka Uturuki kwamba wakimbizi hao watakuwa salama pindi watakaporejea.