1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

KenyaAirways yaishutumu Kongo kuwashikilia wafanya kazi wake

26 Aprili 2024

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways limeutuhumu utawala wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo, kwa unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wake wawili.

Kenya Airways Flughafen Nairobi ARCHIV
Picha: picture-alliance/dpa

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways limeutuhumu utawala wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo, kwa unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wake wawili ambao wanaendelea kuzuiliwa kwa madai ya kukiuka kanuni za forodha, licha ya mahakama kutoa amri ya wafanyakazi hao kuachiliwa huru.

Kenya Airways imesema maafisa wa kijasusi wa jeshi la Kongo, waliwazuwia wafanyakazi hao mnamo Aprili 19 kwa kushindwa kukamilisha kujaza fomu ya forodha ya mzigo uliotarajiwa kusafirishwa. Msemaji wa serikali ya Kongo na wizara ya mambo ya nje ya taifa hilo bado hawajatoa tamko juu ya sakata hilo.

Shirika hilo la ndege la Kenya limesema wakati wafanyakazi wake walipokamatwa mzigo wao bado ulikuwa katika eneo la mizigo, lakini maafisa wa Kongo walidai kwamba walitaka kuondoka bila ya kukamilisha taratibu za forodha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW