1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya:Kaunti zingine 6 hatarini kukumbwa na njaa kali

Wakio Mbogo13 Oktoba 2022

Serikali ya Kenya imezijumuisha kaunti nyingine sita kwenye orodha ya kaunti 29 kati ya 47 zinazohitaji msaada wa dharuda wa chakula kutokana na hali ya ukame inayoendelea kulikumba taifa hilo la pembe ya Afrika .

Kenia Dürre an der Grenze zu Äthiopien
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Serikali imetangaza hatua hiyo katika imezindua wa kituo maalum kitakachoshughulikia usambazaji wa chakula cha msaada kwenye kauti hizo ambazo bado zinaendelea kushuhudia makali ya ukame unaoshuhudiwa.

Kituo hicho kimeundwa na kituo maalum katika bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao kitakachosimamia na kuongoza usambazaji wa chakula cha msaada.

 Katibu wa kudumu kwenye wizara ya mipango maalum, Nelson Marwa amesema kaunti sita zaidi zimejumuishwa kwenye orodha ya kaunti zilizoathiriwa pakubwa na ukame na hivyo kuongeza idadi kufikia kaunti 29.

Soma Pia:Idadi yawanaohitaji msaada wa kiutu Kenya waongezeka

Marwa amesema kuna mawasiliano ya karibu na viongozi wa kaunti ili kuhakikisha wananchi walio na mahitaji wamefikiwa.

"Ikifika inaenda kwa wananchi. Tunafuatilia, kutoka hapa tunapigia Gavana, tunapigia kamishna wa kaunti, tunapigia wahusika wote, kuhakikisha kuwa chakula kinawafikia wananchi."

Alisema Marwa akiainisha namna ambavyo serikali ya Kenya imejipanga katika kufuatilia mchakato wa ugavi wa chakula cha msaada kinachotolewa.

Katikati ya njaa hoja ya lishe shule izingatiwe

Pamoja na hayo, viongozi wanaitaka serikali kutekeleza mpango wa lishe kwa wanafunzi mashuleni kikamilifu.

Imebainika kwamba Watoto wengi kwenye maeneo yaliyoathirika na ukame wanashindwa kuenda shuleni kutokana na makali ya njaa.

Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Viongozi katika maeneo hayo wanabainishwa kwamba, idadi ya watoto ambao wanaogua maradhi ya lishe imeongezeka maradufu ikiwemo, utapiamlo mkali.

Andrew Limaru, chifu wa eneo la Namarei, Kaskazini mwa Kenya, watoto wengi wanatembea umbali mrefuhadi shule huku wakiwa hawajala kitu chochote kutoka majumbani hatua ambayo aliitaja huenda ikaongeza utoro.

"Sasa mtoto anatembea kilomita 15 kuja shule pengine bila kifungua kinywa tena anashinda bila chakula. Itambidi aende atafute chakula hii inaleta shida." Alisema kiongozi huyo.

Soma Pia:UN: Watu milioni 13 wanakabiliwa na njaa kubwa katika eneo la Pembe ya Afrika

Njaa kuwakosesha baadhi mtihani wa taifa

Wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nne wanajiandaa kufanya mitihani yao ya kitaifa mwezi ujao na kuna wasiwasi kwamba baadhi ya wanafunzi kutoka maeneo hayo watakosa kufanya mitihani kutokana na athari hizo za ukame.

Hii inasababishwa na baadhi ya wanafunzi wana uamuzi wa kufanya iwapo watakwenda kutafuta chakula au watahudhuria masomo.

Nadhif Jama, Gavana wa kaunti ya Garisa anamsema endapomamalaka hazitajidhatiti kuchukua hatua za dharura huenda idadi kubwa ya wanafunzi kutoka maeneo hayo wakashindwa kufanya mitihani hiyo muhimu kitaifa.

"Serikali yangu imetenga shilingi milioni 40 ndiposa tuweze kununua maji na chakula kwa haraka.”

Aliweka wazi hatua zilizochukuliwa na mamalaka ili kuhakikisha kila mwanafunzi anahudhuria mitihani, wakati huu ambapo taifa linakabiliana na hali ya njaa katika maeneo kadhaa.

Soma Pia:Afrika Magharibi katika hatari mbaya ya ukosefu wa chakula

Serikali ya kitaifa imesisitiza kuwa ina chakula cha msaada cha kutosha kuweza kufikia miezi tisa ijayo. Tayari shilingi milioni 900 zaidi zimetolewa kwa ajili ya kununua chakula zaidi cha msaada.

Janga la ukame laathiri maeneo ya Kilifi

03:35

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW