1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta akutana na Ruto wakati wa hafla ya maombi

Shisia Wasilwa27 Mei 2021

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto walijipata kwenye jukwaa moja kwa mara ya kwanza baada ya miezi mingi ya kutengana

Kenia President Kenyatta Rede Terroranschläge 02.12.2014
Picha: AFP/Getty Images/S. Maina

Kenyatta na Ruto ambao wanatofautiana kutokana na siasa za urithi za uchaguzi mkuu ujao na Mpango wa Maridhiano maarufu BBI, walihudhuria hafla ya maombi kwa taifa mapema leo.

Maombi hayo ya 18 ya taifa yanajiri huku misuguano ya kisiasa ikizidi kushuhudiwa katika taifa ambalo limebakisha chini ya mwaka mmoja kuandaa uchaguzi mkuu ujao.

Misuguano hiyo imepandisha joto la siasa huku chaguzi ndogo ambazo zilifanyika hivi majuuzi zikidhihirisha utengano kati ya rais na makamu wake.

Ruto ambaye hajaficha nia yake ya kuwania urais ameonesha wazi nia yake ya kutumia chama cha UDA kuwania kiti cha urais kwa kuwaunga mkono wagombea viti mbali mbali kwenye chaguzi hizo mbali mbali kwa tiketi ya chama hicho.

Kwa mara ya kwanza maombi hayo ya taifa yenye kauli mbiu ya mustabali wenye matumaini yalifanyika katika majengo ya bunge huku wabunge 10 na viongozi wengine wakihudhuria. Rais Kenyatta amewataka wabunge kuidhinisha miswada muhimu kwa maslahi ya wakenya.

Mwaka 2019 wakati wa uzinduzi wa mpango wa BBIPicha: AFP/T. Karumba

Rais amenonekana akimpuuza Ruto serikalini, hatua inayolenga kupunguza ushawishi wake serikalini na nje anapojipigia debe ili afanikishe malengo yake ya BBI na kuacha sifa bora atakapaoondoka serikalini.

Kwa upande wake Ruto ambaye anapinga mchakato wa marekebisho ya katiba ameanza kuainisha mipango yake ya kukabiliana na uchumi unaozorota kwa kuonekana akishauriana na wataalamu wa uchumi. Amenukuliwa akisema kuwa serikali yake itajumuisha watu wa viwango vya chini.

Viongozi waliopatiwa nafasi kwenye jukwaa walijitenga na siasa, huku makamu wa rais Ruto akichukua muda kuelezea umuhimu wa ushirikiano.

Maombi kama haya ya taifa yalifanyika miaka miwili iliyopita. Viongozi walielezea changamoto za janga la Corona ambalo lilisambaratisha uchumi huku wito wa ushirikiano ukitolewa kwa viongozi bila ya kujali mirengo ya siasa. Rais Kenyatta amewataka wakenya na viongozi kuzingatia yale yaliyosemwa kwenye hafla hiyo iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW