Afrika Mashariki iendelee kuleta amani Kongo - Kenyatta
13 Julai 2023Kenyatta, ambaye ni msuluhishi katika mzozo huo, aliyasema hayo katika mkutano uliofanyika mjini Goma ambao uliwakutanisha viongozi wa serikali ya Kongo, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa pamoja na wanadiplomasia wa Magharibi.
Soma zaidi: Kagame amtuhumu Tshisekedi kutumia mzozo wa M23 kujinufaisha kisiasa
Rais huyo wa zamani wa Kenya amesisitiza kuwa watu milioni mbili waliolazimika kukimbia mzozo huo wanapaswa kuruhusiwa kurejea salama na lazima uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uheshimiwe.
Soma zaidi: Kenyatta atoa wito wa kupunguza mzozo DR Kongo
Kundi la waasi wa M23, ambalo lilichukua udhibiti wa maeneo kadhaa, linataka mazungumzo na serikali ya Kinshasa ambayo imetupilia mbali azma hiyo.
Badala yake serikali ya Kongo inalitaka kundi hilo kujisalimisha bila masharti na kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda wanaodai wanawasaidia waasi wa M23.