1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta: Awaongoza wabunge kumuaga Kibaki Bungeni

25 Aprili 2022

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza Wakenya kuutazama mwili wa hayati rais mstaafu Mwai Kibaki katika mejengo ya Bunge jijini Nairobi.

Uhuru Kenyatta Präsident Kenia Rede Parlament Nairobi
Picha: Simon Maina/AFP via Getty Images

Waziri wa Usalama wa Taifa Fred Matiang’I amesema kuwa rais huyo mstaafu atazikwa na kupewa heshima zote za kijeshi, baadaye mwili wake utalala katika ikulu kwa siku tatu kabla ya kuzikwa mnamo siku ya Jumamosi. 

Mwili wa hayati Kibaki uliondolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha leo majira wa saa moja asubuhi, huku msafarawake ukipitia katika barabara ya Valley Rd, Kenyatta hadi katika majengo ya Bunge.
 
Ulinzi mkali wa maafisa wa usalama uliimarishwa wakati huo wote, huku Wakenya wakitazama matukio kwa mbali.

 Majira ya saa tatu kamili, Rais Kenyatta akiandamana na mkewe pamoja na naibu wa Rais William Ruto, walifungua safu ya kuanza kuuaga mwili wa hayati Kibaki. 

Soma zaidi:Kipi atakachokumbukwa nacho Mwai Kibaki?

Kibaki ndiye rais wa tatu kupokea heshima kamili ya wanajeshi, huku Rais Kenyatta akiongoza mazishi ya marais wawili wastaafu.

Jeneza la rais mstaafu Kibaki liligubikwa bendera ya taifa huku likisindikizwa na wanajeshi ishara ya mchango wake kwa taifa. 

Kanini Kega ni mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya bunge amesema wataendelea kumuenzi rais Kibaki kutokana na yale ambayo ameyafanya katika taifa hilo la Afrika mashariki.

" Unapopatiwa nafasi ya kuhudumia wananchi jua umepewa nafasi ya kuwafanyiakazi si nafasi ya kujitajirisha"Kanini alinukuliwa na Dw akisema.

Mwili wa Kibaki katika viunga vya Bunge

Kwa siku tatu mwili wa Rais mstaafu utakuwa hapa katika majengo ya bunge, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni ili kuruhusu Wakenya kuutazama. 

Aliekuwa Rais wa Kenya Mwai KibakiPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Siku ya Jumatano mwili huo utapelekwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo kwa ibada ya wafu kabla ya maziko yatakayofanyika nyumbani kwake katika jimbo la Nyeri. 

Tayari serikali imetangaza siku ya Ijumaa kuwa siku ya mapumiko, ambapoibada ya wafu itaandaliwa katika uwanja waNyayo ili kuwaruhusu wakenya kujumuika kumpa heshima zao za mwisho.

Soma zaidi:Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki afariki dunia

 Baadaye Wakenya wataruhusiwa kuuaga mwili wa rais huyo aliehudumu taifa huku akiwa na ndoto kubwa za kuleta maendeleo na kunyanuya ari za wananchi katika kufanyakazi.

Wakenya wamlilia KibakiVox Pop

baadhi ya wakenya katika picha ya pamojaPicha: Dai Kurokawa/epa/dpa/picture alliance

Baadhi ya wananchi wa kenya wameutaja mchango wa hayati kibaki kuwa ni alama ya maendeleo katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Walizitaja hatua zake za kuhakikisha kuwa anannyanyua maisha ya raia kwa kutoa mikopo ambayo iliwasaidia kufanya kazi, hatua iliosababisha vijana wengi kuweza kujiajiri.

Heshima kama hizo za kijeshi zilitolewa kwa mwanzilishi wa taifa Mzee Jomo Kenyatta aliyeaga dunia mwaka 1978 na rais wa pili wa taifa hayati Daniel Arap Moi aliyefariki dunia mwezi Februari mwaka 2020.

Soma zaidi:Kenya: Viongozi watoa wito wa kuvumiliana kisiasa

Kibaki aliaga dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 90 baada ya kuugua. Bendera zimekuwa zikipeperushwa nusu mlingoti kote nchini tangu wakati huo hadi siku ambayo atakapozikwa.

Kibaki Aliongoza Kenya kwa mihula miwili kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2013. Atazikwa karibu na mkewe mama Lucy Kibaki, nyumbani kwake Othaya, jimbo la Nyeri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW