SiasaChina
Waziri mkuu wa zamani wa China Li Keqiang afariki dunia
27 Oktoba 2023Matangazo
Kituo cha utangazaji cha CCTV kimearifu kwamba Li Keqiang aliyekuwa mapumzikoni jijini Shanghai katika siku za karibuni alipata shambulizi la ghafla la moyo jana Alhamisi na jitihada za kunusuru maisha yake hazikufanikiwa na hatimaye kufariki majira ya mapema hii leo, Ijumaa.
Keqiang aliyekuwa na miaka 68 amefariki ikiwa ni miezi 10 baada ya kustaafu shughuli za kiserikali. Alikuwa waziri mkuu na kiongozi wa baraza la mawaziri chini ya rais Xi Jinping kwa miaka kumi hadi alipojiuzulu mwezi Machi.
Keqiang anakumbukwa kama kiongozi aliyependelea mageuzi, tofauti na wenzake wanaopenda kuonyesha misimamo mikali na kutobadilika.