Kerry aendeleza ushindi wake Marekani
15 Februari 2004Matangazo
WASHINGTON: Nchini Marekani Seneta wa Kidemokrasi John Kerry ameendeleza orodha ya ushindi wake katika chaguzi ndogo mikoani. Alishinda uchaguzi katika mji mkuu Washington na mkoani Nevada kwa wingi mkubwa dhidi ya wapinzani wake. Hivi sasa Seneta Kerry amekwisha shinda chaguzi 14 kutoka jumla ya chaguzi 16 ndogo kwa niaba ya chama cha kidemokrasi,na kuongeza nafasi zake za kuchaguliwa kuwa mgombea wa Chama cha Kidemokrasi katika uchaguzi wa Rais hapo mwezi wa Novemba dhidi ya Rais George W. Bush.
