1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi dhidi ya Katumbi yapelekwa mbele ya korti ya katiba

Oumilkheir Hamidou
11 Oktoba 2018

Kesi inayomkabili Moise Katumbi ya kuwaajiri mamluki imefikishwa katika korti ya katiba.

Moise Katumbi kongolesischer Oppositionsführer
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Gosset

Kesi ya mgombea kiti cha rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya  Kongo anaeishi uhamishoni, Moise Katumbi kwa madai ya kuwaajiri mamluki, imesitishwa na kufikishwa mbele ya korti ya katiba-wakili wake amesema.

Uamuzi huo unaoweza kufifisha matumaini yake ya kugombea kiti cha rais uchaguzi utakapoitishwa Disemba mwaka huu, umepitishwa baada ya masaa manne ya kusikiliza ushahidi bila ya kuwepo mahakamani wahusika wote wawili, Katumbi aliyewahi kuwa gavana wa mkoa wa Katanga na raia wa Marekani Darryl Lewis anaetuhumiwa kuwa mamluki.

Mmojawapo wa mawakili wa watuhumiwa hao Jean-Joseph Mukendi wa Mulumba amesema majaji wamekataa kusikiliza hoja zao kuhusu kutokuwepo mahakamani wateja wao.

Jean Joseph Mukendi ameongeza kusema utaratibu katika korti ya katiba unaweza kudumu miezi isiyopungua mitatu na kwa namna hiyo kurefusha kesi hiyo  hadi baada ya uchaguzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW